Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wafanyakazi NMB watoa mil. 11 matibabu ya watoto JKCI
Afya

Wafanyakazi NMB watoa mil. 11 matibabu ya watoto JKCI

Spread the love

WAFANYAKAZI wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya Benki ya NMB, wameikabidhi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya Dar es Salaam, Sh 11 milioni kusaidia kulipia gharama za matibabu ya watoto wenye uhitaji wanaotibiwa kwenye taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia, wametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh1.7 milioni kwa wodi ya watoto ya Hospital ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Dk. Yona Kabata (kushoto) vilivyotokana na michango ya wafanyakazi wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya benki hiyo. Wa tatu kushoto ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Sista Barian Ngona, Meneja Mikopo ya Nyumba Benki ya NMB, Miranda Lutege (wa pili kulia) na Meneja Mahusiano Mwandamizi NMB, Pendo Massawe (wa tatu kulia).

Kwa nyakati tofauti tarehe 19 Desemba 2023, Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite, alikabidhi kwa niaba ya wafanyakazi hao, hundi ya mfano ya kiasi hicho kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi JKCI, Dk Robert Aloyce na vifaa tiba hivyo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Dk. Yonna Kabata.

Akizungumza wakati wa hafla ya jijini Dar es Salaam, Ngingite, alibainisha kiasi walichotoa kimetokana na michango ya wafanyakazi wa Idara hiyo na nyongeza kutoka benki yake, lengo likiwa ni kugusa maisha ya wenye uhitaji katika jamii, ambapo hufanya hivyo kila mwisho mwaka kupitia idara mbalimbali na Ofisi za Matawi yao kote nchini.

“Kwa niaba ya wafanyakazi wenzetu, tuko hapa kutoa kiasi cha Sh11.57 milioni kilichotokana na michango ya mishahara yetu na nyongeza kutoka taasisi yetu, lengo likiwa ni kugusa maisha ya watoto wenye uhitaji wanaotibiwa hapa. Tunajua matatizo ni mengi na wenye uhitaji ni wengi, lakini tukaona tuje hapa kusaidia wachache kati yao.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Dk. Yona Kabata (kushoto) vilivyotokana na michango ya wafanyakazi wa Idara ya Wateja Wadogo na Biashara ya benki hiyo. Wa pili kushoto ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Sista Barian Ngona, Meneja Mikopo ya Nyumba Benki ya NMB, Miranda Lutege (wa pili kulia) na Meneja Mahusiano Mwandamizi NMB, Pendo Massawe (wa tatu kulia).


“Tumaamimi kwa kiasi hiki tunachokabidhi, tutakuwa tumeyagusa na kuokoa maisha ya watoto walio katika ‘stage’ mbalimbali za matibabu hapa JKCI, ili waweze kufanyiwa upasuaji na baada ya hapo tunawaombea uponaji wa haraka kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kawaida.

 “Hii yote ni kusapoti uwekezaji mkubwa ulilofanywa na Serikali katika Sekta ya Afya, tumepita idara mbalimbali kujionea hilo na sisi kama wadau tukajiona tunao wajibu na uwezo wa kuunga mkono hilo.

 “Tumekuwa tukifanya hivi kila mwisho wa mwaka kwa wafanyakazi wa benki yetu kupitia Idara na Ofisi za Matawi kote nchini kujichanga mishahara yao na kuangalia maeneo ya kusaidia iwe kwa mayatima ama wagonjwa kama hivi,” alibainisha Ngingite.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa taasisi hiyo, Dk. Delila Kimambo, aliishukuru NMB kwa msaada waliotoa kwa watoto hao wanaotibiwa na taasisi yake na kwamba, kiasi hicho kinaenda kugusa pakubwa mioyo na maisha ya wanufaika miongoni mwa watoto wanaotibiwa hapo.


“Mlichofanya hapa ni jambo kubwa, mmewapa watoto hawa na wazazi ama walezi wao, mwisho mzuri wa mwaka, tayari kwa kuingia mwaka mpya na matumaini mapya.

 “Kwa niaba ya watoto hawa, sisi JKCI tunawashukuru wafanyakazi wote na NMB kwa ujumla kwa kuisapoti Serikali ambayo imefanya uwekezaji mkubwa sana hapa unaopaswa kuungwa mkono na wadau wa afya kama hivi mlivyofanya nyie” alisema Dk. Delila.

 Kwa niaba ya watoto wengine, Pili Khalfan wa Maneromango mkoani Pwani, ambaye ni mama mzazi wa mmoja wa watoto walionufaika, alisema msaada huo umekuja kwa wakati, kwani alielemewa na gharama za matibabu kiasi cha kukata tamaa, hasa baada ya kutengwa na ndugu pamoja na kukimbiwa na baba wa mtoto wake.

 “Naishukuru sana NMB kwa kunipa aina hii ya msaada, ambao sikuutarajia na sitousahau maishani mwangu. Nimeteseka sana, sikuwa na msaada wowote, hata ndugu walinitenga, huku baba wa mtoto wangu naye akinikimbia.

 “Nimekuwa napata wakati mgumu, kulala kwangu shida, kula yangu na mtoto ni shida. Aliwahi kutokea mfadhili wa kusaidia matibabu ya mtoto, lakini bima aliyokatiwa tukaambiwa ni ndogo, hivyo haitoshi kugharamia upasuaji wa moyo.

“Leo NMB inaenda kunifuta machozi mimi na mwanangu kusaidia gharama za matibabu yake. Naitakia mafanikio yaliyotukuka benki hii, ili iweze kuendelea kusaidia wenye uhitaji wengi zaidi,” alisema Pili wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wazazi na walezi wenzake.

 Kutoka Kisarawe, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dk Yonna John Kabata, hakusita kuipongeza NMB kwa msaada wa vifaa tiba, ambavyo sio tu vitawasaidia watoto hospitalini hapo, bali pia utawapa wepesi katika kuhudumia makundi ya watoto wanaotakiwa kufanyiwa oparesheni (surgery cases) na wale wanaohitaji matibabu ya kawaida (treatment cases).

 “Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali na wagonjwa wote, nitumie nafasi hii kuwashukuru sana NMB kwa msaada huu wa vifaa tiba, ambavyo mnaweza kuona ni mdogo, ila niwahakikishie ni mkubwa na huenda ingetuchukua muda mrefu kuvipata.

“Hapa zipo baadhi ya huduma za bure kwa watoto, lakini wahitaji ni wengi, hivyo huongeza changamoto ya kuishiwa vifaa na mwingine kuvikosa. Hii isiwe mara ya mwisho, mtukimbilie kila mtapokuwa na fungu la kusaidia, itaokoa maisha ya wagonjwa wetu,” alisema Dk. Kabata, mbele ya Muuguzi Mfawidhi, Sista Barikian Ngona na Muuguzi wa Wodi ya Watoto, Flora Mchaina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!