Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waumini wamefanya maombi kulaani vibaka
Habari Mchanganyiko

Waumini wamefanya maombi kulaani vibaka

Spread the love

Waumini wa makanisa, mtaa wa Sanare kata ya Daraja mbili Jijini Arusha, wameungana na kufanya maombi ya pamoja kulaani vibaka wanaosumbua mtaani hapo kutokana na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ubakaji huku viongozi wa mtaa huo wakiwa kimya kufumbia macho vitendo hivyo. Anaripoti Joseph Ngilisho, Arusha…(endelea).

Waumini hao wakiongozwa na Mwinjilisti Evance Minja wa kanisa la KKKT usharika wa Ungalimited, jijini Arusha walidai hawaoni haja ya kuwa na viongozi wakati wameshindwa kutatua kero dhidi ya vibaka wanaosumbua mtaani hapo kwa matukio ya wizi, matusi, ulevi, ubakaji, ulawiti, matumizi ya dawa za kulevya na uuzaji wa  bangi na mirungi hadharani.


Akitoa mahubiri katika maombi hayo huku wakinyeshewa na mvua Mwinjilisti Minja aliiomba serikali ya mtaa huo itoe tamko iwapo imeshindwa kukomesha uhalifu mtaani hapo, ili waweze kuingilia kati kwani wanaamini Mungu hashindwi kwa lolote katika vita hiyo.

“Katika maombi haya tumewaalika viongozi mbalimbali akiwemo Diwani Prosper Msofe, Mwenyekiti wa mtaa, Afisa Mtendaji wa kata, polisi kata na wengine lakini hakuna hata mmoja aliyefika kuwa na sisi hii inaonesha wazi kwamba hawapo na sisi,” alisema.

Baadhi ya waumini hao Rehema Mbeswa kutoka kanisa la KKKT usharika wa Ungalimited na Margaret Philipo wa kanisa Katoliki la Moyo safi Ungalimited, walisema wameamua kufanya maombi hayo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupambana na uhalifu kwa njia za kiroho.

Alisema wameamua kumlilia Mungu baada ya kuona jitihada za viongozi wa serikali ya mtaa kudhibiti vibaka hao zimeshindikana huku wananchi wakizidi kuteswa na makundi hayo ya uhalifu yanayosumbua mtaani hapo usiku na mchana bila kuchukuliwa hatua.

“Lengo kuu la kukutana hapa ni kwa ajili ya kumlilia mungu kutokana na matukio ya uhalifu yanayofanywa na magenge ya uhalifu yanayotishia maisha yetu ili Mungu akatende muujiza wa kuwabadilisha vijana hao na mtaa wetu na mitaa ya jirani waondokane na uhalifu”

Naye kiongozi wa jumuiya wa kanisa katoliki Ungalimited,  Salvador Makoi alisema mtaa huo wa Sanare umekuwa kitovu cha uhalifu kutokana na makundi ya uhalifu kutoka mitaa mbalimbali kufanya mtaaa huo kama kambi yao ya uhalifu.

Makoi alimtaka Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo kuhamishia makazi yake huko ili ajionee adha na karaha ya vibaka hao, ambapo jeshi la polisi na uongozi wa kata hiyo limeshindwa kuwadhibiti

Aliishauri serikali ya mtaa huo kufanya jitihada za ziada katika kukabili makundi hayo ya uhalifu ikiwemo kuishirikisha serikali ya wilaya na mkoa ili wananchi waweze kuishi kwa amani kwani kwa sasa wamekuwa hawalali au kupata usingizi kutokana uhalifu unaoendelea mtaani hapo.

Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Aaron Samweli aliwatoa hofu waumini hao kwa kuwataka wawe watulivu kwani serikali haitashindwa na tayari jitihada zimefanyika za kuwakabili vibaka hao.

Aliwataka wananchi kutokuwa waoga kutoa ushirikiano ikiwemo kuwataja wahusika na kutoa ushahidi pale wanapohitajika mahakamani.

“Kuna kikao tulikaa na RPC na kila mtaa tumekabidhiwa askari polisi lakini tatizo la huu mtaa wananchi hawatoi ushirikiano wa kuwataja wahalifu”

Alisema jitihada zimefanyika ikiwemo kuchukua majina ya vijana wanaosumbua kwa uhalifu ambao wanatukana watu wazima matusi ya nguoni  akidai yanafanyiwa kazi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano bila woga kuwafichua wahalifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!