SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuwapunguzia mzigo wa kodi wafadhili wa miradi ya maji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Ushauri huo umetolewa leo Alhamisi tarehe 6 Mei 2021, na Mbunge wa Ndanda (CCM), Cecil Mwambe wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.
“Sasa hivi tunapata misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kupata visima na network ya usambazaji mabomba, kumekuwa na malalamiko kidogo kwamba mara nyingi wanapoleta vifaa Tanzania kwa ajili ya kusaidia watu wenye haja ya maji,” amesema Mwambe.
Mbunge huyo wa Ndanda amesema “inapofika kwenye maeneo kwa ajili ya kuvi-clear (kuvitoa) wanatozwa kodi nyingi sana kana kwamba wanafanya biashara wakati wanaleta misiaada ya michango ya wafadhili huko kwao, waziri angalia utaratibu wa kurekebisha tozo.”
Akichangia hotuba hiyo, Mwambe amesema changamoto hiyo iansababisha nchi kukosa misaada ya miradi ya maji.
“Badala ya kuwatoza gharama kubwa pesa hiyo ingeweza kuleta visima katika maeneo mbalimbali,” amesema Mwambe.
Leave a comment