May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COVID-19 India: ‘Lockdown’ ndio muafaka pekee

Spread the love

 

RAHUL Gandhi, kiongozi wa chama cha upinzani cha Congress nchini India, amesema njia iliyobaki kuisaidia India kutokana na kuzama katika maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19), ni kujifungia ‘lockdown.’ Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Amesema, tayari Serikali ya India imefeli kwenye mifumo na mbinu zake zote katika kukabili kusambaa kwa maambukizi ya virusi hivyo, na kwamba serikali haina uwezo tena.

“Kujifungia ndani ndio njia pekee ya muafaka iliyobaki kwa sababu, serikali imefeli kabisa katika mbinu na njia zake,” amesema kiongozi huyo alipoulizwa na shirika moja la Habari la kimataifa.

Katika saa 24 zilizopita, India imeweka rekodi mpya ya kufikisha vifo 3,980 huku maambukizi yakiwa zaidi ya 400,000.

Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India alieleza kuwa na hofu ya ‘kufungia nchi hiyo kwa wasiwasi wa kuvuruga uchumi wake. Wiki iliyopita alisema atafikia uamuzi huo ikiwa ndio hatua ya mwisho ya kuokoa taifa hilo.

Mji wa Uttar Pradesh wa tatu kwa watu wengi (200 milioni) nchini India, umeanza kutekeleza ataratibu wa kutotoka ndani kwa siku tano -mpaka Ijumaa.

Mji wa kwanza kwa watu wengi, Maharashtra na wa pili kwa idadi ya watu Bihar tayari wameanza kujifungia ikiwa ni hatua za awali za kukabiliana na virusi hivyo.

India imepokea jumla ya dozi 160 milioni, imepokea msaada wa mitungi ya gesi ya Oxygen na vifaa vilivyohusu corona kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani na mataifa mengine.

Mpaka kufikia leo tarehe 6 Mei 2021, maambukizi ya corona duniani yamefika watu 155,926,028, vifo 3,258,339 na waliopona
133,391,798.

error: Content is protected !!