Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa mazingira watakiwa kuunga mkono utunzaji wa mazingira
Habari Mchanganyiko

Wadau wa mazingira watakiwa kuunga mkono utunzaji wa mazingira

Spread the love

 

WADAU wa mazingira mkoani hapa wametakiwa kuunga mkono utunzaji wa mazingira hasa suala la upandaji miti sababu utunzaji wa mazingira ni sawa na kutunza uhai wa watu. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Hayo yalisemwa jana na Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Jackob Ole Mameo wakati wa kampeni ya upandaji miti pembezoni mwa bwawa la Mindu iliyoandaliwa na balozi wa mazingira Taifa Chage Alex Chage kwa kushirikiana na KKKT na wadau wengine wa mazingira.

Askofu Mameo alisema suala la upandaji miti pia ni kustawisha mazingira sababu kwa sasa mvua zimeadimika na hata zikiwepo zinakuwa hazina uhakika.

Alisema kanisa linawafundisha kila jambo linawezekana mbele za Mungu sababu suala la kuhifadhi mazingira pia ni la Mungu hivyo anaimani hawawezi kushindwa kama wakishirikiana vizuri ambapo wataweza kuleta mabadiliko chanya hata ya hali ya hewa tofauti na sasa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa aliwaomba wakazi wa maeneo Jirani na Bwawa hilo na waishio Manispaa na mkoa wa ujumla kuendelea kutunza vyanzo vya maji huku akiwasihi viongozi wa dini kuendelee kuhamasisha kuhusu mazingira na kufanya wananchi kuthamini mazingira.

Alisema Serikali imejipanga kwamba kila nyumba inapaswa kupandwa miti mitano hivyo ni matarajio yake kwamba kila mmoja atalizingatia hilo ikiwemo kampeni ya soma na miti ili kuwafanya Watoto wapende na kuipanda miti sababu misitu ni uhai.

Aidha Mwassa alisema zaidi ya 80% ya wakazi wa Morogoro wanategemea bwawa na mindu kupata maji na sasa Serikali inakwenda kulitanua ili wananchi wote tupate maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 50 ijayo bila matatizo.

Naye Mratibu wa Kampeni hiyo ya upandaji miti Balozi wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Chage Alex Chage alisema suala la utunzaji wa mazingira ni wajibu wa kila mmoja katika jamii kwa kushirikiana na sekta binafsi Pamoja na Serikali.

Alisema zaidi ya miti 500 imepandwa katika eneo kuzunguka bwawa la Mindu ambapo kampeni ya upandaji miti inaendelea katika ameneo mengine ili kusaidia kukua kwa hamasa ya uhifadhi wa mazingira.

Mmoja wa wadau wa Mazingira aliyeshiriki kampeni hiyo Meneja wa Shirika la kikristo la kuhudumia wakimbizi nchini (TCRS) Rehema Samwel alisisitiza jamii kuona haja ya kuwa mstari wa mbele katika suala zima la utunzaji mazingira wakianza na kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka.

Samwel alisema suala la upandaji miti linalosisitizwa na viongozi wa Serikali, dini na wadau wa mazingira ni jambo jema linalopaswa kuzingatiwa lengo likiwa ni kuboresha uhifadhi wa mazingira na kuiepusha jamii katika hatari ya kuwa na maeneo jangwa au nchi kukosa kabisa mvua licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi yanayojionesha kwa sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!