MHUBIRI mwenye utata wa kanisa la Good News International lililopo kaunti ya Kilifi Malindi, Kenya na mkewe Rhoda Mackenzie pamoja na watuhumiwa wengine 16 wamefikishwa katika mahakama ya Shanzu nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Mhubiri huyo na wafuasi wake wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ugaidi baada ya mahakama ya Malindi Kaunti ya Kilifi kuwachilia huru na kisha kukamatwa tena ambapo hadi sasa Mackenzie anahusishwa na vifo vya watu takribani 100.
Uchunguzi wa miili ya watu hao umebaini kuwa huku njaa ikionekana kuwa chanzo kikuu cha vifo, baadhi ya waathiriwa wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa, au kukosa hewa.
Waendesha mashtaka wanaomba kumshikilia Mackenzie, ambaye alianzisha Kanisa la Good News International Church mwaka wa 2003, kwa siku nyingine 90 hadi uchunguzi utakapokamilika.
Jana Alhamisi Ezekiel Odero,mhubiri maarufu wa televisheni New Life International lililopo Mavueni Kaunti ya Kilifi, , aliachiwa huru kwa dhamana ya KSh. 1.5 milioni.
Odero pia atakuwa akisubiri rufaa aliyoikata ya kutaka huduma za Kanisa lake zilizozuiliwa ziweze kuendelea na Serikali iondoe zuio la akaunti zake za Benki ilizozifunga..
Awali, upande wa Mashtaka uliiomba Mahakama indelee kumshikilia Mchungaji huyo kwa siku 30 zaidi, ukidai unaendela kukamilisha upelelezi dhidi ya mtuhumiwa na kwamba uwepo wake nje unaweza kuharibu ushahidi.
Leave a comment