Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa Habari wapeleka bunge mapendekezo yaliyoachwa Muswada wa Habari
Habari Mchanganyiko

Wadau wa Habari wapeleka bunge mapendekezo yaliyoachwa Muswada wa Habari

Deus Kibamba
Spread the love

 

WADAU wa Haki ya Kupata Habari nchini (CoRI), wametinga bungeni jijini Dodoma, kwa ajili ya kuwasilisha kwa wabunge mapendekezo yao yaliyoachwa nje kwenye Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wakizungumza jijini humo leo tarehe 24 Aprili 2023, wajumbe hao wa CoRI wamesema wanaamini wabunge watayapokea mapendekezo hayo kisha kuyawasilisha wakati Muswada huo ukijadiliwa bungeni ili yaingizwe.

Mjumbe wa CoRI, Deus Kibamba, amesema wamekusudia kuzungumza na wabunge ili kuwaeleza umuhimu wa mapendekezo yao juu ya marekebisho ya baadhi ya vifungu ambavyo vinalalamikiwa kuwa kandamizi, kuingizwa katika Muswada huo.

Naye James Marenga, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN), amesema wamemua kukutana na wabunge kwa kuwa wao ndiyo watunga Sheria na kwamba Muswada huo umeshafikishwa mikononi mwao.

“Tulianza na Serikali wakatusikiliza wakawasikisha kile walichowasilisha bungeni, ni wakati sasa na sisi kukutana na wabunge kwa ufafanuzi zaidi. Naamini ni waelewa watatuelewa,” amesema Marenga.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, Neville Meena, amesema “ni suala la kawaida pale panapokuwepo na hatua ya utungwaji wa Sheria Taasisi husika ikawa inatoa ufafanuzi zaidi juu ya kile inachopigania. Tumeona ni fursa kwetu kukutana na wabunge ili kuwaeleza tunapigania nini na kwa nini.”

Hivi karibuni Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, alisema CoRI ni muhimu kukutana na wabunge ili kushawishi baadhi ya vipengele vilivyoachwa kwenye Muswada huo.

Miongoni mwa vipengele ambavyo CoRI wanapenda viingizwe kwenye muswada wa sheria kabla ya kujadiliwa ni pamoja na sehemu ya saba inayohusu adhabu na makosa yake ambapo walipendekeza kupungua adhabu hasa kwa makosa yanayohusu kitaalamu.

Walipendekeza serikali iondoe ukomo wa chini wa adhabu kwa vifungu vyote kwa kuwa inambana hakimu au jaji kuamua vinginevyo.

Na kwamba, sheria nyingi kwenye mataifa yaliyoendelea zinaweka ukomo wa juu wa adhabu kwa kuwa inatoa fursa kwa jaji au hakimu kutoa adhabu kulingana na mazingira ya kesi husika.

Pia wanaeleza kifungu cha 7(2) kinaeleza kuwa serikali inaweza kutoa agizo habari fulani kuchapisha au kutangaza habari kwa kuwa ina umuhimu kwa Taifa CoRI wanaeleza, kifungu hicho ni kuingilia uhuru wa uhariri kwa kuwa, uhariri unafanywa nje ya chumba cha habari ambacho kina watu wenye weledi na uzoefu mkubwa.

CoRI wanalalamikia kifungu cha 5(e)a,b kinachohusu utoaji wa leseni ambapo Mkurugenzi wa Habari (Maelezo), anaweza kukataa maombi ya leseni au kuhuisha kulingana na matakwa yake.

Pia kinampa mamlaka ya kusitisha leseni wakati wowote anapoona chombo husika hakina mwenendo anaoutaka yeye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!