Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji wadogo waliodaiwa ‘wavamizi’ wamwangukia Biteko
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji wadogo waliodaiwa ‘wavamizi’ wamwangukia Biteko

Spread the love

 

WACHIMBAJI wadogo wa Madini ya Dhahabu katika Kijiji cha Mwasabuka Kata ya Iyenze wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wamelalamikia kitendo cha kutimuliwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Jamhuri William katika eneo hilo la machimbo. Anaripoti Paul Kayanda, Geita … (endelea)

Uamuzi huo wa Mkuu huyo wa wilaya umetokana na madai ya wachimbaji hao kuvamia eneo lenye leseni ya mwekezaji kampuni ya Barrick inayomiliki Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyopo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya vyombo vya habari jana tarehe 29 Oktoba, 2021 baadhi ya wachimbaji hao, Salvatori Augustino na Patrick Laphael walidai kushangazwa na tamko la mkuu huyo wa wilaya aliyewapa siku saba kuondoka katika machimbo hayo.

Walisema kwa sasa hali ya wachimbaji wadogo ni mbaya kwa sababu baada ya kuvumbua madini katika eneo hili amejitokeza mwekezaji mkubwa na kudai hilo eneo ni la leseni yake.

“Kwa kweli kitendo hiki ni kutufukuza kama mbwa mwitu kwenye eneo tulilogundua dhahabu wenyewe, kwenye eneo hili linalodaiwa ni leseni ya Barrick kuna migodi mingi na huu tulipo hauna hata mwezi tangu tuanze uchimbaji sasa kwanini watuondoe sisi? alihoji Salvatori Augustino..

Waziri wa Madini, Dotto Biteko

Mchimbaji mwingine David Juma alidai kuwa huenda kuna mwekezaji mwingine anahitaji kipande hicho kinachoonekana kuwa na dhahabu ndio maana sasa wanafukuzwa

“Tuna muda mrefu tunazama katika maduara haya na wanatuangalia bila kuhoji chochote, kwa kweli ili kututendea haki sote tunatafuta, tunamuomba Waziri wa Madini, Doto Biteko afike kutugawia maeneo haya,” alisema.

Aidha, wachimbaji hao waliomba serikali kufidia hasara waliyopata kwa kuwa waliwekeza fedha zao zaidi ya milioni tisa katika uchimbaji huo.

Hata hivyo, akijibu malalamiko hayo wachimbaji hao mkuu huyo wa wilaya alisema eneo la Mwasabuka lina leseni ya Barrick na serikali ina hisa 16 kupitia kampuni ya Twiga.

Alisema Barrick wanaendesha shughuli zao kwenye eneo hilo hivyo, wachimbaji hao walivamia eneo hilo.

“Ni kweli nimewapa siku saba waondoke katika eneo hilo kwamba wamuachie Barrick aendelee na shughuli zake katika eneo hilo.

“Lakini wachimbaji hawa nimewapa maelekezo na kuondoka hapa sio kwamba waende sehemu tofauti ndani ya wilaya hii kuna maeneo mengi ambayo ni rasmi kwa uchimbaji mdogo na ni lazima wafuate utaratibu na sheria za madini wasikae kulaumu,” alisema William.

Alisema hii ni mara ya pili kwa wachimbaji hao kurudi kwenye eneo hilo.

Kwa upande wake Afisa Madini mkazi wa Mkoa wa madini Mbogwe, Mhandisi Joseph Kumburu alisema wachimbaji hao wamefukuzwa baada ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 10 za mrabaha.

“Viongozi wa eneo hilo wanagawa mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu ya mrabaha na kumpa mtu ambaye hahusiki na Ofisi ya Madini. Sasa waliohusika tunawasaka ili kuwakamata na kuwafungulia kesi,” alisema Kumburu.

Pia Kumburu alisema kwenye wilaya hiyo kuna changamoto ya utoroshaji mawe hayo bila kibali kwani mpaka sasa kuna kesi 30 za utoroshaji bila kibali cha ofisi ya madini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!