RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa tayari kuanza shughuli za kawaida ifikapo Januari 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Uganda … (endelea).
Katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa juzi jana tarehe 29 Oktoba, 2021 amesema hatua ya hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa chanjo za Covid-19.
Museveni amesema machifu na maofisa wengine wa serikali wanapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata chanjo katika maeneo yao.
Amesema kufikia Desemba 2021, nchi itakuwa imepata dozi milioni 23 za chanjo ya Covid-19.
“Hii itatosha kuwachanja watu milioni 12, ikiwa ni pamoja na makadirio ya wafanyakazi milioni 4.8 wa mstari wa mbele na watu walio hatarini, na kutuweka kwenye njia ya kufungua nchi kikamilifu,” amesema.
Pia amesema shule zitafunguliwa mwezi Januari mwakani bila kujali kama watu watakuwa wamechanjwa au lah, na kuongeza kuwa uamuzi utakuwa mikononi mwao.
“Niko hapa kuwaambia Waganda wote kwamba chanjo kwa wafanyakazi wote walio mstari wa mbele sasa zinapatikana. Tembea hadi kituo cha afya, ubebwe na bazukulu au nenda kwa baiskeli.”
Leave a comment