Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Viwanja 14 kuuzwa kwa mnada Dodoma
Habari MchanganyikoTangulizi

Viwanja 14 kuuzwa kwa mnada Dodoma

Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili katika Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru
Spread the love

HALIMASHAURI ya  Jiji la Dodoma linakusudia kuuza viwanja  maalum 14 kwa njia ya mnada utafanyika siku ya Alhamisi 10 Januari mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili katika Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa viwanja hivyo ni kwa ajili ya biashara kwa wawekezaji ambao watakuwa wanahitaji kupata mahitaji muhimu ya viwanja hivyo.

Alisema viwanja ambavyo vinatarajiwa kuuzwa kwa njia ya Mnada vitakuwa na matumizi ya Vituo vya kuuza mafuta, kituo cha afya na matumizi mengime maalumu kwa wale ambao watahitaji kuwekeza.

Katika hatua nyingine Mafuru alisema kuwa wale watakakao kuwa tayari kununua viwanja hivyo watatakiwa kufika katika ofisi za Jiji kwa zamani zilikuwa ofisi za manispaa  tarehe 8 Januari mwaka huu kwa ajili ya kwenda kuvikagua viwanja hivyo kabla yam nada.

Alisema kuwa siku yam nada wanunuzi watatakiwa kulipa asilimia 25 ya manunuzi na baadaye watalazimika kulipa na kumalizia fedha yote ndani ya siku 14 kwa maana ya wiki mbili.

“Mnunuzi atalazimika kulipia asilimia 25 ya mauzo ya kiwanja na baadaye ndani ya wiki mbili atalazimika kuwa amemaliza kulipia fedha yote, hii ni kutokana na kuhakikisha kila aliyenunua kiwanja anakuwa mnunuzi halisi na siyo dalali.

“Kumekuwepo na taratibu za madalali kuvamia minada na kununua viwanja au bidhaa mbalimbali ambazo zinauzwa katika mnada na badala yake madalali wamekuwa wakitafuta wateja wengine jambo ambalo linasababisha kuwepo na mlolongo mkubwa, kutokana na hali hiyo sasa tutahakikisha tunawathibiti nadalali katika kufanya biashara ya jinsi hiyo,” alisema Mafuru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!