December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wazee wa Chadema: Muswada wa vyama vya siasa, kaburi la demokrasia

Hashim Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema

Spread the love

MUSWADA wa Vyama vya Siasa waendelea kupingwa na vyama vya upinzani nchi kwa kilichotajwa kuwa kaburi la Demokrasia. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Vyama vya upinzani nchini vimeungana kupinga muswada huo wanaodai kuwa umelenga kuua demokrasia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Hashim Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema amepigilia msumali wa kupinga muswada huo kwa kile alichoeleza umelenga kukipanga nguvu chama tawala na kuua vyama vya upinzani.

“Kuna athari kubwa kwenye nchi hii kukikosekana, sisi tunakosoa Serikali inapokosea,” amesema Juma.

Amesema kuwa Muasisi wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere alikubaliana na mfumo wa vyama vingi kwa sababu alijua kuwa chama tawala kikiwa chenyewe hakitaweza kuwajibika.

Akitoa mfano wa wabunge wa Upinzani walipaza sauti zao kupinga sheria kadhaa ambazo zingekuwa maumivu kwa wananchi amemtaja Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini kuwa alipaza sauti yake kuwatetea wastaafu kwenye sheria ya kikokotoo cha asilimia 25 kwenye pensheni ya wastaafu.

Amesema kuwa hakuna mbunge yoyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeweza kutetea na kupaza sauti juu ya kikokotoo hiko.

Juma amesema kuwa ifike mahala watanzania wajue umuhimu wa kuwepo kwa wapinzani nchini.

error: Content is protected !!