Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025
Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the love

NGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi wake ili wahakikishe chama hicho kinapata ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetokewa leo tarehe 23 Septemba 2023, wakati Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam,  inazindua makala inayoonyesha kazi ilizofanya Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu (Machi 2022-Septemba 2023), mkoani Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, Dorothy Semu amewataka vijana wajipange kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizozipita,ili wapate ushindi.

“Uchaguzi wa 2019 tumeona Vyama vyetu viligomea, 2020 tumeona na nataka kuwakumbusha vijana kwamba ushindi hautokei tu, ushindi unapangwa na unatengenezwa na mikakati inayotekelezeka,” amesema Semu na kuongeza:

“Tujiandae vizuri ili yale yaliyotungima ushindi wetu 2020 tuyavuke, safari hii ushindi Wetu tuulinde mara dufu bila kuogopa na kuvunja sheria lakini kutumia mbinu zenye akili. Tujiandae kutumia mbinu zenye akili.”

Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Joran Bashange, amewataka vijana wa chama hicho kuwa wabunifu ili kulinda kura.

“Siasa ya Sasa ni za ushindani, ukitaka siasa za enzi zetu huambulii kitu. Lazima muwe wabunifu lakini kama mnataka siasa za kutegemea niwe mbunge, diwani na hujui unaingiaje unapoteza muda. Inabidi muweke mpango mkakati mwaka huu kupeleka uchaguzi ujao mkifanya hivyo uwezo wa kushinda ni mkubwa,” amesema Bashange.

Naye Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Dar es Salaam, Renatus Pamba, amewataka viongozi wa vijana katika majimbo, kufanya kazi kubwa ya kuwahamasisha vijana wengine wajiunge na chama hicho.

“Kazi hii inayofanywa na ngome mkoa ikawe chachu kwa viongozi wa majimbo kufanya kazi ili kuvutia vijana wengine wajiunge na ACT-Wazalendo,” amesema Pamba.

Makamu Mwenyekiti Ngome Vijana ACT-Wazalendo Bara, Selemani Misango amesema “vijana tuachane na siasa nyepesi tunazofanya sasa za kusema sana kuliko vitendo. Tuwandae vijana wetu wakajua kwamba tunapokwenda katika chaguzi zilizo mbele yetu tuwe tayari kwa lolote ili CCM watuachie ushindi wetu.”

“CCM wanapaswa kuona kwamba kuna watu wanataka ushindi wao, wasipoliona Hilo wanauwezo wa kutupa tume huru na katiba mpya lakini wakiona udhaifu uko eneo hili na wakatuadhibu,” amesema Misango.

Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Chamwenyewe, ameitaka ngome hiyo iongeze hamasa ili vijana washiriki katika uchaguzi pamoja na kulinda kura.

“Hamasa zisiishie hapa, tutengeneze vijana watakaokomboa nchi kupitia uchaguzi. Tutengeneze vijana watakaopambana sio wavaa tai na suti, watakaopambana ili tupeane mbinj za kushinda katika uchaguzi sababu hatuwezi kushinda mezani tunashinda kwa Kupambana,” amesema Chamwenyewe.

Naye Katibu wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Twaha Rashid, amesema kazi kubwa inabidi ifanyike ili kuwaamsha vijana kupigania nchi Yao kupitia uchaguzi, kwani asilimia kubwa ya kundi hilo limejikita katika masuala ya kucheza kamali na Michezo mingine badala ya kulinda taifa lao.

“Safari ya kushika dola ni ngumu Kwa aina ya Vijana tulionao, wanaokaa vijiweni , kubeti na kufuatilia mpira wa miguu. Hamasa kubwa inatakiwa ifanyike,” amesema Rashid.

Mwanachama mpya wa ACT-Wazalendo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Marwa Wankaba, amesema “kushinda ni kutangazwa, tusikubali kushinda peke yake bali kutangazwa. Hata ukipata kura asilimia 90 ya kura kama hujatangazwa wewe si mahindi. Ngome ya vijana ni nguzo ya chama hivyo ijipange kwa uchaguzi ujao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!