Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vichwa 3 vya treni ya umeme, mabehewa 27 yatua
Habari Mchanganyiko

Vichwa 3 vya treni ya umeme, mabehewa 27 yatua

Spread the love

Shirika la Reli Tanzania limepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 30 Disemba 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano (TRC), Jamila Mbarouk imesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajli ya uendeshaji wa reli ya kwango cha kimataifa – SGR.

Amesema mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya Sung Shn Roling Stock Technology’ (SSRST) ya nchini Korea Kusind.

Ameongeza kuwa mabehewa matatu yaliyosalia yanatarajwa kuwasili nchini Februari, 2024. Vichwa 13 viliyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu kama ituatavyo, vichwa sita vitawasili mwezi Machi na vichwa saba vitawasili Aprili, 2024.

“TRC itaanza kupokea Seti ya kwanza kati ya Seti 10 za treni za Kisasa (EMU) mwezi Machi 2024 Mei seti 2, Juni seti 2. Julai set 2. Septemba seti 2 na seti ya mwisho mwezi Oktoba 2024.

“Vichwa vilivyopokelewa, kiutendaji vina mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa. Mabehewa 27 katika madaraja ya Uchumi na Biashara.

“Daraja la biashara (Business class) ni mabehewa 13, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 45 na mabehewa ya daraja la Uchumi (Economy cdass) ni 14, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimatata kumuwezesha abiria kusafiri wa amani na salama,” amesema.

Amesema Shirika la Relı Tanzania linaendelea kupokea kwa awamu vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kmataifa (SGR).

Aidha, amesema zoezi la majaribio ya vitendea kazi linaendelea kwa mujibu wa mkataba ili kuhakikisha vinaendana na mifumo ya miundombinu iliyojengwa nchini kabla ya kuanza uendeshaji wa kibiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!