Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Upungufu wa umeme wabaki 218 MW kutoka 421 MW
BiasharaHabari za Siasa

Upungufu wa umeme wabaki 218 MW kutoka 421 MW

Spread the love

Serikali imesema hali ya upatikani umeme nchini imeimarika na sasa upungufu wa umeme umebakia 218 MW. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga,  tarehe 9 Novemba, 2023 Jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge  waliotaka kufahamu mpango wa Serikali katika kumaliza changamoto za umeme nchini.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kijibu maswali bungeni Jijini Dodoma, kuhusu mpango wa Serikali wa kumaliza tatizo la umeme nchini, tarehe 9 Novemba, 2023.

Amesema, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeendelea kupunguza upungufu wa umeme nchini kutoka MW 421 hadi MW 218 na hivyo kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Aidha, Naibu Waziri Kapinga ameeleza zaidi kuwa, pamoja na jitihada hizo, Serikali pia imeongeza uzalishaji wa gesi katika visima vya Mnazi Bay, Somanga na Madimba ili kuweza kuongeza gesi ya kuzalisha umeme na kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

Vilevile inaendelea na matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme ili kuboresha zaidi Hali ya Upatikanaji wa Umeme nchini.

Pia ameagiza Mameneja wa TANESCO, kuweka utaratibu mzuri wa mgawo wa umeme katika taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi ikiwemo vituo vya afya, ofisi za serikali, shule na n.k ili wananchi waendelee kupata huduma.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Christine Ishengoma aliyetaka kufahamu kumalizika kwa tatizo la umeme katika Manispaa ya Morogoro, Kapinga, amesema Serikali imefunga mashineumba yenye uwezo wa MVA 120 katika Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msamvu ili kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme kwa mkoa huo.

Kapinga alifafanua kuwa, kazi hiyo ya kufunga mashineumba itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 10.5 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba 2023.

Kuhusu usambazaji wa umeme katika taasisi za elimu, afya, dini, pamoja na visima, Kapinga amesema tayari miradi inaendelea ya kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ambapo wigo wa usambazaji wa umeme huo umeongezwa kutoka kilomita moja hadi mbili  ili Taasisi nyingi ziweze kufikiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!