Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko DC Ilala aunda tume kuchunguza vibanda vya wamachinga Kivule kubomolewa
Habari Mchanganyiko

DC Ilala aunda tume kuchunguza vibanda vya wamachinga Kivule kubomolewa

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Ilala (DC), Edward Mpogolo, ameunda timu kwa ajili ya baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wanaodaiwa kuvamia na kubomoa vibanda vya wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga), katika maeneo ya Kivule, kisha kupora mali zao kinyume cha sheria. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mpogolo amesema hayo jana Alhamisi, alipofika katika maeneo ya wamachinga kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao, baada ya tukio hilo kutokea usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 5 Novemba 2023.

Alisema timu hiyo kazi yake ni kuchunguza waliohusika na tukio hilo, kisha kuwachukulia hatua ikiwa sambamba na kulipa fidia wamachinga dhidi ya athari walizowasababishia.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Edward Mpogolo.

“Kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na cha kihuni, hakifai kuvumiliwa, bahati nzuri niliongea na kamanda wa polisi alinihakikishia hakuna askari aliyetumwa kuja huku. Niliongea na mkurugenzi hakuna ambaye alimtuma kuja huku, maana yake sheria lazima iwahusu,” alisema Mpogolo na kuongeza:

“Nitaunda timu itakuja kushughulikia changamoto hi na yule atakayebainika simuachi. Haiwezekani mtu anatafuta fedha kwa shida leo hii anatokea mtu mwingine anachukua mali zake kinyume cha sheria.”

Awali, akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao, Bihimba Mpaya, alidai baada ya kujitoa mstari wa mbele kuwatetea wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakisumbuliwa mara kwa mara, baadhi ya viongozi wa kata ya Kivule, walimtishia kwamba watamfungulia kesi ya uhujumu uchumi.

“Nilikuwa naambiwa nitafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi sababu mimi kimbelembele natetea watu. Naomba Mkuu wa wilaya utusaidie matatizo haya yaishe,” alisema Bihimba.

Baadhi ya wafanyabiashara walimueleza Mpogolo kuwa, kitendo cha kubomolewa vibanda vyao kinatokana na baadhi ya viongozi wa kata hiyo ambao wanawalazimisha kwenda katika soko ambalo wao wanakodisha vizimba kwa gharama kubwa kwa ajili ya kujinufaisha.

Walidai kuwa, mfanyabiashara ili apate kizimba katika soko hilo, anatakiwa alipie kiasi cha Sh. 300,000 kila mwezi.

Mbali na kuambiwa walipe gharama kubwa, walidai soko hilo miundombinu yake si rafiki kwa wao kufanya biashara na hata wateja kuingia. Huku wakiweka wazi kwamba, wako tayari kuhamia sokoni endapo changamoto hizo zitatatuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

error: Content is protected !!