Tuesday , 5 December 2023
Kimataifa

Unyama wa polisi Kenya

Polisi wakimburuza mtuhumiwa kwa pikipiki
Spread the love

POLISI watatu nchini Kenya, wamekamatwa kwa tuhuma za kumfunga kamba Mercy Cherono (21) kwenye pikipiki, kisha kumburuza kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Mercy ametuhumiwa kushirikiana na watu wengine kuvunja na kuingia kisha kuiba vitu mbalimbali katika nyuma moja ya polisi katika Mji wa Olenguruone, Nakuru uliopo kilometa 250 Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Nairobi.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inaonesha polisi mmoja akiwa amepanda pikipiki, akimburuza binti huyo. Wakati akifanyiwa unyama huo, mtu mmoja alionekana kumtandika bakora, huku binti huyo akiomba asitendewe kitendo hicho. Tukio hilo linaelezwa kutokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Binti huyo alikimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa ikiwa ni pamoja na kuvunjwa mguu. Mara kwa mara nchini Kenya, polisi wamekuwa wakituhumiwa kuwatesa raia.

“Kwa kweli sijui hata niliponaje,” Mercy amenukuliwa na gazeti la Standard la Kenya. Suruali na gagulo lake, vyote vilivutwa chini karibu na magoti yake huku akiburuzwa kwenye barabara hiyo iliyo na vumbi.

“Niliwaomba waniachie, lakini hakuna hata mmoja aliyesikia kilio changu,” Mercy aliliambia gazeti hilo akiwa kitandani Hospitali.

Lee Kinyanjui, Gavana wa Nakuru amewaambia waandishi wa habari Jumatano wiki hii kwamba, kile kilichoonekana kwenye video hiyo, hakiwezi kuvumilika

“Hivi vitendo vya kikoloni vinazidi kupaka rangi nyeusi jeshi letu. Polisi lazima wawajibike kwa kufikishwa katika vyombo vya sheria,” gazeti la the Daily Nation limemnukuu Kinyanjui.

Kitengo cha makossa ya jinai nchini humo kimeeleza, polisi hao watu wanashikiliwa katika kipindi hiki ambacho uchunguzi unaendelea.

Karibu watu 15 wameuawa kwenye maandamano yaliyolenga kupinga kuendelea kujifungia ndani ili kukabili kusambaa kwa virusi vya corona.

Taarifa zaidi zinaeleza, polisi hao hata walipokamatwa kwa tuhumaza mauaji, hawajafanywa lolote na zaidi wameachwa huru.

Yassin Moyo (13), ni miongoni mwa raia wa nchi hiyo aliyeuawa. Msemaji wa jeshi hilo Charles Owino aliuambia mtandao wa BBC, kwamba kijana huyo aliuawa kwa bahati mbaya wakati polisi wakilikabili kundi la watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!