Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge CCM wajaa hofu kutemwa
Habari za Siasa

Wabunge CCM wajaa hofu kutemwa

Spread the love

BAADHI ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameingia hofu ya kutorudi bungeni, kutokana na muundo wa mchakato wa kuteuliwa ndani ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

CCM kama vilivyo vyama vingine vya siasa, kinatarajia kufanya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa udiwani, ubunge na urais kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, baada ya bunge kuvunjwa tarehe 19 Juni 2020.

Albert Obama, Mbunge wa Buhigwe mkoani Kigoma na Joseph Kakunda Mbunge wa Jimbo la Skonge mkoani Tabora (CCM), ni miongoni mwa wabunge walioonesha wasiwasi wa kutorudi bungeni, kutokana na baada ya baadhi ya makada wa chama hicho CCM kuonesha nia ya kutaka majimbo yao.

Wakizungumza kwa wakati wakati wanachangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2020/2021 leo tarehe 12 Juni 2020, bungeni jijini Dodoma wabunge hao walirusha mashambulizi kwa watu waliojitokeza katika kinyang’angiro hicho.

Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, amekuwa tishio kwa Obama, baada ya kuonesha nia ya kutaka kugombea jimbo lake la Buhigwe.

Waziri Mpango ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais, jana tarehe 11 Juni 2020, akiwa bungeni jijini Dodoma, aliwaomba wananchi wa Buhigwe, wamchague ili awe mmoja kati ya watumishi wa Rais John Magufuli.

Kauli hiyo imemuibua Obama na kujihami kwamba, ana amini wananchi wa Buhigwe wataendelea kumchagua, kutokana na imani yao kwake, kufuatia utendaji wake uliopelekea kuondoa changamoto zao.

Mbali na Obama, Kakunda naye aliutumia ukumbi wa bunge, kutoa tahadhari kwa baadhi ya watu walioanza harakati za kulitaka jimbo lake la Skonge. Kakunda amewataka watu hao kutomfanyia vurugu katika jimbo lake.

“Ndugu zangu, Sikonge najua kuna vijana wangu na wazee wanapita pita huko wanataka jimbo, mimi kama mtu muungwana ambaye nililelewa vizuri, nawakaribisha wapite jimboni lakini wasifanye vurugu, sisi tunataka tumalize uchaguzi wetu vizuri bila kupigana ngumi,” alisema Kakunda na kuongeza:

“Wale ni WanaCCM ndugu zangu wapokelewe, mtu anakwenda kusalimia mjomba wake, shangazi wake huwezi kumkataza, mimi naomba uchaguzi wa amani ambao utakuwa wa mfano mkoani Tabora.”

Kakunda alimaliza maelezo yake kwa kumpongeza Spikawa Bunge, Job Ndugai, kwa kuendesha vizuri shughuli za mhimili huo.

Baada ya Kakunda kumwaga sifa hizo, Spika Ndugai aliwaondoa wasiwasi wabunge wa CCM, kwa kuwaahidi kwamba atamaliza utaratibu wote, ingawa hakutaja ni utaratibu wa aina gani.

Spika Ndugai aliwataka wabunge hao kuacha midomo, na kusema kama walivyopitisha azimio la kumpongeza bungeni, na yeye atalipa fadhila zake.

“Nashukuru kwa mchango wako na hasa ulivyomalizia kwa kumsifu mtani wako, tunaendelea na uchangjiaji lakini niwambie kwamba kwa utaratibu uleule na juzi mmepitisha azimio la kunipongeza, na mimi  niwahakikishie kuhusu utaratibu niachie jamani, tatizo lenu mdomo, mmenielewa, niachie mdomo funga,” amesisitiza Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!