Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Afya Ujerumani, Tanzania zaingia makubaliano ya afya
Afya

Ujerumani, Tanzania zaingia makubaliano ya afya

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitatu na serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kuimarisha afya ya msingi nchini. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo leo tarehe 12 Septemba 2019, Dk. Zainabu Chaula, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema, wizara yake imesaini mkataba huo na serikali ya Ujerumani katika kuboresha sekta ya afya katika maeneo manne ambapo sekta hiyo itapata kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 26.6.

Dk. Chaula amesema, kwa mwaka huu wameweka makubaliano ili fedha hizo zitolewe kwa wakati mmoja na kuweza kutumia mfumo wa Force Akaunti, kama walivyoweza kutumia kwenye ujenzi wa Vituo vya afya na Hospitali za Wilaya na Mikoa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

“Tumeanza mahusiano tangu mwaka 1961, kuanzia  mwaka 2003 huu ni mkataba wa tano na mkataba wao ni wa miaka mitatu mitatu ambapo umejikita katika kuimarisha afya ya msingi katika halmshauri zetu katika vituo vya afya pamoja na zahanati,” amesema.

Ametaja maeneo yatakayonufaika na mkataba huo ni uhimarishaji wa taarifa, afya ya mama na mtoto, uzazi wa mpango, bima ya afya kwa akina mama wajawazito pamoja na utawala bora jinsi ya kutumia fedha hizi kulingana na kanuni na taratibu za nchi.

“Huu ni muendelezo wa mkataba wa miradi mingi ambayo tumeifanya katika kuboresha sekta ya afya, kama mnavyokumbuka hadi sasa hivi tumeshafanyia ukarabati wa vituo vingi vya afya ambapo tuna vituo 470 ambavyo vimeshafanyiwa ukarabati  tangu mwaka 2017 katika ngazi za zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya.

Aidha, Dk. Chaula alisema Serikali iliwekeza shilingi bilioni mia moja na milioni mia tano katika hospitali za halmashauri.

“Zamani hawa wenzetu walikua wakitumia wakandarasi wao na pesa wanakaa nazo, hivyo tumekaa nao na kukubaliana kama fedha hizi watazitoa kwa wakati mmoja ili tuweze kuzisimamia kama tulivyofanya kwenye vituo tulivyoanza ili kuweza kutekeleza kwa umakini na kupata matokeo makubwa katika kipindi hiki,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi GGML wajitokeza kuchunguzwa saratani

Spread the loveWAFANYAKAZI wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) leo...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML yatoa msaada wa vifaa tiba kuboresha afya Geita

Spread the loveKATIKA jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya afya mkoani Geita,...

Afya

Hospitali Kanda Mtwara yaokoa mamilioni, yajipanga kuhudumia nchi jirani

Spread the love  MAMILIONI ya fedha yaliyopaswa kutumika katika kusafirisha wagonjwa kutoka...

AfyaHabari Mchanganyiko

Magonjwa yasiyoambukiza tishio, vyombo vya habari vyatakiwa kuelimisha umma

Spread the loveVYOMBO vya habari vimetakiwa kuongeza jitihada katika elimu ya kujikinga...

error: Content is protected !!