Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli amfuta kazi Mkurugenzi Mkuu TISS
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli amfuta kazi Mkurugenzi Mkuu TISS

Spread the love

RAIS wa Jamhuri, Dk. John Pombe Magufuli, amemfuta kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Dk. Modestus Kipilimba. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu), jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, tarehe 12 Septemba 2019, imeeleza kuwa nafasi ya Kipilimba imechukuliwa na Kamishena wa Polisi, Diwani Athuman Msuya.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishena Diwani Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).

Taarifa hiyo iliyotolewa na Gerson Msigwa, ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, haikueleza sababu za rais kumfuta kazi Kipilimba.

Akizungumza baada ya kumuapisha kushika nafasi hiyo, Rais Magufuli, amemtaka Kamishena Diwani Athuman kuchapa kazi “kwa kuweka mbele maslahi ya taifa,”

Uteuzi wa Kamishena Diwani umeanza leo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais amesema, Dk. Kipilimba atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya kufanywa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, tarehe 6 Septemba 2018, Kamishena Diwani Athumani alikuwa katibu tawala mkoa wa Kagera.

Alichukua nafasi ya ukurugenzi mkuu wa Takukuru, kutoka kamishena mwanzake wa Polisi, Valentino Mlowola, ambaye sasa amefanywa kuwa Balozi.

Kamishena Diwani Athuman amepata kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!