UPANDE wa serikali umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa wapo katika hatua za mwisho kufunga ushahidi wao kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma mjini, anakabiliwa na kesi ya uchochezi Na 327 ya 2018 anayodaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu Uvinza, Kigoma.
Leo tarehe 12 Septemba 2019, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, amedai kuwa upande huo ulijipanga kufika na shahidi wa 13 lakini amepata dharura hivyo hakuweza kufika mahakamani.
Katuga amedai, wana mashahidi watatu ambapo shauri hilo likipangiwa tena, wataweza kufunga ushahidi wao .
Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 7, 8, na 9 Oktoba 2019.
Leave a comment