November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi wenyeviti wa CCM wilaya kuanza Oktoba mosi

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka

Spread the love


KATIBU wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Shaka Hamdu Shaka amewasisitiza wanachama wa chama hicho kujitokeza kwenye uchaguzi wa ngazi ya Wilaya tarehe 1 na 2 Octoba, 2022.  Anaripoti Helena Mkonyi. TUDARCo … (endelea).

Uteuzi huo wa mwisho wa  wagombea uwenyekiti  wa wilaya  katika Wilaya 168 nchini,  umefanyika leo Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan.

Shaka amesema “Tumeteuwa na tumeshapata wagombea ambao wataenda kusimama kwenye uchaguzi wa ngazi ya Wilaya tarehe 1 na 2 Ockoba 2022”.

Shaka amewaomba wanachama wajitokeze kwa wingi  katika uchaguzi wa wenyeviti wa CCM ngazi ya Wilaya ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa katiba yao.

Aidha amesema kwamba Halmashauri kuu ya Taifa imeongeza muda wa kuchukua fomu na kurejesha fomu kwa ngazi ya Taifa na Mkoa kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara.

error: Content is protected !!