Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu 2020: NEC yabebeshwa tuhuma mpya
Habari za Siasa

Uchaguzi Mkuu 2020: NEC yabebeshwa tuhuma mpya

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inalaumiwa kubagua vyama vya siasa vya upinzani. Ni katika maboresho ya kanuni mbalimbali za uchaguzi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2 Juni 2020, Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amedai “NEC imepanga kuharibu uchaguzi.”

Amesema, hatua ya NEC kufanya mabadiliko bila kushirikisha wadau wake, kinalenga kuibua mkanganyiko na hatimaye kuvuruga uchaguzi.

Na kwamba, mchakato huo uliendeshwa kwa haraka na kisha kulazimisha vyama kusaini rasimu ya kanuni hizo. ACT-Wazalendo iligoma kusaini.

“Sisi kama ACT tuligoma lakini tukatishiwa kuwa, tusiposaini hatutoruhusiwa kufanya kampeni kwenye za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020,… zoezi hili limeendeshwa kwa tume kulazimisha kilichoaanda,” amesema Ado.

Amesema, NEC ilitoa muda mchache wa kujadili kanuni hizo ilikwepa majadiliano na wadau wa uchaguzi kwa kutorejesha rasimu ya mwisho iliyobeba mawazo ya wadau.

“Wenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage aligusia kuwa, mchakato wa kukusanya maoni kwa ajili ya marekebisho ya kanuni za uchaguzi (Madiwani, Wabunge na Urais ), umefanyika, na NEC ipo mbioni kuzikamilisha .

“NEC inakusudia kufanya hivi bila kuwepo kwa kikao cha wadau kujadili rasimu ya mwisho ya kanuni husika,… kwanini NEC inakwepa majadiliano na wadau?” amehoji.

Ameainisha upungufu wa vipengele wa kanuni hizo ni pamoja na wasimamizi kutowapa hati ya kiapo mawakala wa vyama vya siasa, na kuweka utaratibu wa uchaguzi kutuma orodha na utambulisho wa mawakala kwa wasimamizi wa vituo.

“Kwa uzoefu, utaratibu huu utatumika kuwahujumu mawakala wengi wa vyama vya upinzani .Tunafahamu kuwa, uchaguzi haukamiliki bila kuwepo kwa mawakala, hiki kilitokea Kinondoni,” amesema Ado.

Amesema, katika kanuni hizo, kipo kipengele kinawataka wamawala kutopewa nakala za matokeo ya uchaguzi “kanuni ya 56(2), inasema kuwa nakala zitatolewa iwapo kutakuwa na nakala za kutosha …NEC haikujiandaa kwa uchaguzi.”

Ado amesema kuwa, kanuni hizo zimewaziba midomo waangalizi wa uchaguzi kwa kuwaalika kwa hiyari waangalizi wa nje..”kanuni hizo zinakata waangalizi kuripoti kwa waandishi wa habari upungufu wa uchaguzi.”

Katibu mkuu huyo wa ACT-Wazalendo ameitaka NEC kushirikisha kikamilifu wadau wa uchaguzi, kabla ya kukamilisha kwa kanuni hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!