Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi 2020: Maalim Seif aitesa CCM Zanzibar
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi 2020: Maalim Seif aitesa CCM Zanzibar

Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimeonesha wasi wasi wake juu ya harakati za Maalim Seif  Shariff Hamad, za kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akizungumza na wanachama wa chama hicho visiwani Pemba,  jana tarehe 1 Machi 2020, Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, amehoji kitendo cha Maalim Seif kugombea urais katika kila uchaguzi.

Polepole amehoji kuwa, kwa nini Maalim Seif hazuiwi kugombea urais, ili kutoa nafasi kwa wanachama wengine kugombe nafasi hiyo, kama inavyofanywa na CCM.

“Katika uchaguzi wa mwaka 1995 alikuwepo, mwaka 2000 alikuwepo, 2005 alikuwepo , 2010 alikuwepo na mwaka 2015 alikuwepo. Samahani kidogo, kwenye chama chake yuko peke yake au yuko na wenzie?” amehoji Polepole na kuongeza:

“ Unajua unaweza kuwatukana wenzio bila matusi, sijui wenzake wanashindwa vipi kumng’amua. Unakuja uchaguzi anawaambia nisikilizeni mimi, unakuja uchaguzi mwengine nisikilizeni,  wengine wako wapi?”

Wakati huo huo, Polepole amesema visiwani humo kwa sasa hakuna upinzani, kutokana kwamba serikali ya CCM inatatua kero na shida za wananchi, zilizosababisha wananchi visiwani humo kuwa na kinyongo dhidi ya chama hicho..

 “Hapa pemba hakuna upinzani, hapa Pemba kuna tatizo la kuchelewa kushughulika kero za watu, mpaka ikafikia wakati wananchi wana kinyongo. Kinyongo wakapeleka kwa watoto wao, lakini nakuhakikisha hapa Pemba kwa mwendo huu tunaoenda nao kwa kushughulika na kero na shida  za watu wetu . Hapa hakuna upinzani,” amesisitiza Polepole.

Maalim Seif ambaye kwa sasa amehamia katika Chama cha ACT-Wazalendo akitokea CUF, hajaweka wazi kama ana mpango wa kugombea urais visiwani Zanzibar.

Mara kadhaa alipohijiwa na wanahabari kuhusu suala hilo, alijibu kwamba, hana mpango huo, ila kama atapata baraka za wananchi na chama chake atagombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!