April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru: CCM msifurahie kufukuzwa kwa Membe

Spread the love

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amewataka wanachama wa CCM kutosherehekea uamuzi huo na kuwataka kuweka akiba ya maneno, kufuatia kumfukuza uanachama, Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu. Anaripoti Regina Mkonde,Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi leo tarehe 2 Machi 2020 jijini Dar es Salaam, Dk. Bashiru amesema kupoteza mwanachama ni msiba na si sherehe,  si jambo la kufurahia.

Amesema wamechukua hatua hiyo baada ya hatua za awali kushindwa kufanikiwa, huu ni uamuzi mgumu, na si kusherehekea na nisingependa WanaCCM kujitokeza hadharani kufurahia.

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, milango ya CCM  kupokea wanachama wanaokiri makosa yao na kuomba msamaha iko wazi, hivyo Membe anaweza kukata rufaa juu ya suala hilo.

“Mchakato huu ni kama wa kimahakama kuna rufaa, nikianza mimi kusema wakati mimi ndio nitapokea rufaa kama nipo ni kama naingilia mchakato wa haki. Na matarajio yangu ni kwamba atarudi CCM, nikiwa hai au nimekufa.

“Sababu milango ya kuwapokea wanachama iko wazi na kuondoka iko wazi, mimi nimesaini barua za misamaha 14 na niko tayari kusaini ya Membe kurudi kama akitaka,” amesema Dk. Bashiru.

error: Content is protected !!