Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa leo Jumapili amesema katika mikataba hiyo mitatu, serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DP World ambazo zitaongeza mapato na zitapunguza gharama za uendeshaji. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Amesema hapo awali serikali imekuwa ikitumia takribani asilimia 90 ya mapato yote yaliyokusanywa katika uendeshaji wa maeneo yanayokodishwa na kubakia asilimia 10 tu.
Amesema kutokana na mikataba hiyo serikali itaweza kubakia na asilimia 60 ya mapato yote ya maeneo ambayo yanakodishwa kwa DP World.
“Faida ya mapato kwa serikali inatokana na maboresho ya huduma za bandari kupitia uwekezaji huu pia itaonekana kwa kiwango cha juu kwenye ukusanyaji wa ushuru unaofanywa na TRA pamoja na mamlaka nyingine zilizopewa jukumu la kukusanya ushuru, tozo na ada mbalimbali katika shehena zinazohudumiwa na bandari ya Dar es Salaam,” amesema.
Leave a comment