Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema katika kutekeleza mkakati wa Serikali wa kuimarisha shughuli za bandari Dar es Salaam, Serikali inasaini mikataba mitatu ambayo haihusishi shughuli zote za bandari za Dar es Salaam wala bandari nyingine za Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)
Mikataba hiyo iliyosainiwa leo Jumapili Ikulu jijini Dodoma ni mkataba wa nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba nne hadi saba na mkataba wa gati namna sifuri hadi tatu ambazo zitaendeshwa kwa pamoja kati ya TPA na DP world kwa shughuli za kibiashara na zile za serikali.
Kwa upande wa gati 8-11 tayari tumeanza mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine. Na kama kutakuwa na sifa ambazo tunaziona bora zaidi hivyo kutakuwa na mwendeshaji mwingine na wala sio DP World.
Leave a comment