Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Biashara TPA: TRA itakusanya trilioni 26.7 bandarini
BiasharaTangulizi

TPA: TRA itakusanya trilioni 26.7 bandarini

Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar
Spread the love

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa leo Jumapili amesema kwa kawaida Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hukusanya tozo kutokana na meli 90 zinazohudumiwa kwa mwezi na uboreshaji utakapofanyika kupitia kampuni ya DP World wataweza kuhudumia meli 130. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akitoa taarifa kuhusu mikataba mitatu iliyosainiwa leo Ikulu jijini Dodoma, amesema mapato yaliyokuwa yanakusanywa na TRA yataongeza kutoka Sh tirilioni 7.8 ambazo zinakusanywa eneo la bandari peke yake kwa mwaka 2021/2022  hadi kufikia trilioni 26.7 itakapofika mwaka 2032.

Amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi sio kitu kipya katika mkataba huo ambao ni wa aina yake.

Amesema mkataba huo umezingatia changamoto za serikali kupitia mkataba wa awali kati ya TPA na TICTS ambao ulikoma tarehe 31 Disemba mwaka 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Mwenge

Spread the love  KAMPUNI ya Meridianbet imefika maeneo ya Mwenge jijini Dar-es-salaam...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Biashara

Serengeti yakabidhi mkwanja kwa mshindi wa Maokoto ndani ya Kizibo

Spread the love Mshindi wa Maokoto ndani ya kizibo kutoka Kahama Mjini...

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!