Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Biashara Wakali wa muziki kutoka Tanzania, Kenya, na Uganda wakutananishwa kwenye jukwaa moja
BiasharaMichezo

Wakali wa muziki kutoka Tanzania, Kenya, na Uganda wakutananishwa kwenye jukwaa moja

Spread the love

 

KWA mara yakwanza nchini Tanzania, Serengeti Lite Oktobafest ilileta pamoja vipaji vya muziki na ubunifu wa hali yajuu wa Afrika Mashariki katika fukwe za Dar es Salaam, ikitoa burudani na kuonyesha utamaduni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tukio hili la kipekee lilijumuisha safu ya wasaniimaarufu, ikiwa ni pamoja na Nyanshiski kutoka Kenya, Jose Chameleon kutoka Uganda, Ali Kiba, Bill Nas, Chino, G Nako, na wabunifu kama vile MakekeInternational kutoka Tanzania, wote wakishirikianakwenye jukwaa moja kugusa mioyo ya maelfu yaWaafrika Mashariki.

Esther Raphael, Meneja wa Chapa kwa Serengeti Lite na Serengeti Premium Lager, alisema. “Serengeti Lite Oktobafest si tu maadhimisho ya muziki na utamaduni; ni jukwaa linalowawezesha vijana wa Afrika Masharikikupata fursa za biashara,” alisema. “Zaidi ya hayo, tamasha hili linaonyesha jinsi bia inaweza kutumikakama daraja, kuwaunganisha tamaduni na watumbalimbali wa Afrika Mashariki kwa lugha ya muziki.”


Moja
ya mambo ya kipekee zaidi ya tamasha hilililikuwa jinsdi ilizingatia usafi wa mazingira. RispaHatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu, alielezea fahari yake katika juhudi za tamasha kwakuzingatia utunzaji wa mazingira. “Serengeti Lite Oktobafest ilikuwa tamasha lenye kutunza mazingirabila taka zozote, ambapo mazingirayalipewakipaumbele,” alielezea. “Timu yetu ya waokota taka ilifanya kazi kwa bidii kuhakikisha mazingira safi nikila wakati wakati wa tamasha.”

Pamoja na hayo, usalama ulikuwa ni kipaumbele cha juu, huku waandaaji wa tamasha wakishirikiana naUber, wakitoa punguzo la asilimia 40 kwa watuwanaenda kwenye tamasha kwa safari za kwenda nakurudi Coco Beach. Hatua hii ililenga kuzuia hatarizinazohusiana na uendeshaji wa magari wakiwawamelewa, kuhakikisha kuwa washiriki wote walikuwana njia salama na ya kuaminika ya usafiri.

Vipaji vilivyoonyeshwa katika jukwa la Serengeti lite vilikua ni vya kipekee na hakika watu waliburudika naaonyesho ya wasanii yaliyogusa mioyo ya hadhira nakudhirisha utajiri wa tofauti za kitamaduni za Afrika Mashariki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Pesa ipo huku Meridianbet, beti sasa

Spread the love  WIKIENDI inaishia leo hii jaman kama bado hujasuka mkeka...

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Mwenge

Spread the love  KAMPUNI ya Meridianbet imefika maeneo ya Mwenge jijini Dar-es-salaam...

Biashara

Serengeti yakabidhi mkwanja kwa mshindi wa Maokoto ndani ya Kizibo

Spread the love Mshindi wa Maokoto ndani ya kizibo kutoka Kahama Mjini...

Biashara

Ushindi rahisi unpatikana kila ukicheza kasino ya Hot Joker

Spread the love  HOT Joker Fruits 20 ni mchezo wa sloti ya...

error: Content is protected !!