Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tulia: Tauche kuendekeza majungu tuchape kazi
Habari za Siasa

Tulia: Tauche kuendekeza majungu tuchape kazi

Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson amewataka Wananchi kuacha tabia za kuendekeza majungu na badala yake wajikite katika kujenga Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Dk. Tulia ameyasema hayo leo Jumamosi Disemba 24, 2022 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 kwa Wajumbe wa Mkutano mkuu maalum wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Tughimbe.

Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wasiopenda maendeleo wanapoona Viongozi wakiwemo wakitaifa wakifanya kazi nzuri kwa jamii wao wanapambana kutengeneza majungu na kukosoa utendaji ili kuleta mkanganyiko usio na faida kwa jamii.

Amewataka Wananchi wakiwemo wa Jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono katika majukumu yake ili aweze kuwatimizia mahitaji yao ikiwemo uboreshaji wa miundombinu, elimu, afya n.k kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Humphrey Nsomba ambao wamempongeza Dkt. Tulia kwa namna ambavyo ameweza kufanya mabadiliko ya maendeleo ya haraka katika Jimbo hilo kwa kipindi chake kifupi cha Uongozi.

1 Comment

  • Asante ndugu tulia.sisi wanambeya tunakupongeza kwa kazi kubwa unayofanya ktk jimbo na kitaifa wale wapiga majungu wanahasara kubwa ya kimaisha na wala wasikupe shaka sisi tuko nyuma yako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

error: Content is protected !!