Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko MECIRA yapongeza hatua za Rais Samia kulinda vyanzo vya maji
Habari Mchanganyiko

MECIRA yapongeza hatua za Rais Samia kulinda vyanzo vya maji

Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)
Spread the love

 

KITUO cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA), kimemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kukazia maagizo ya Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, juu ya kuondolewa kwa wananchi wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji katika vyanzo vya maji, ili kukabiliana na ukame. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumamosi, tarehe 24 Desemba 2022 katika mkutano wa MECIRA uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema maagizo hayo yatasaidia kuwaamsha wanaoharibu vyanzo vya maji kwamba hawako juu ya Sheria.

Wasaidizi wa Rais Samia wameshaanza kutekeleza agizo hilo ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda mkoani Morogoro kushughulikia tatizo hilo katika Bonde la Kilombero.

Aidha, Balile ameiomba Serikali izingatie misingi ya haki za binadamu katika kuwandoa wananchi wanaofanya shughuli katika vyanzo vya maji hususani katika Bonde la Ihefu na Usangu, mkoani Mbeya.

“Tunajua kuna watu wamewekeza miundombinu wengine wana mashine za kukoboa mpunga hivyo uhamishaji wao lazima uendane na ubinadamu sababu tunafahamu athari zitakazotokea. Wengine wana miaka 10 hadi 12 wapo muda mrefu wapewe walau mwaka mmoja kuvuna mazao waliyolima na wapigwe marufuku wasifanye shughuli tena katika kipindi hicho,” amesema Balile.

Katika hatua nyingine, ameshauri Serikali kutekeleza azma yake ya kugawa vitalu vya Bonde la Rufiji kwa ajili ya kilimo, kwa wananchi pindi mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, utakapokamilika.

Mwenyekiti huyo wa TEF, amesema vyanzo vya maji vikilindwa vitasaidia nchi kupata umeme wa uhakika utakaosaidia kuimarisha uchumi wa nchi kupitia kilimo cha umwagiliaji na shughuli za uzalishaji viwandani.

Naye Mwenyekiti wa MECIRA, Habib Mchange, amesema kituo hicho kinampongeza Rais Samia kwa agizo la kuwoandoa watu wanaovamia hifadhi za maji “tuna kila sabahu ya kumpongeza Rais Samia Kwa usikivu wake wa haraka.”

Mchange amesema MECIRA kitaendelea kusimamia ulinzi wa rasilimali za nchi bila kuogopa vitisho, huku akitoa wito kwa asasi za kiraia na vyama vya siasa kushirikiana katika kulinda mazingira.

“Sisi MECIRA tunasema tutakwenda nalo uraro uraro juu ya wanaoharibu mazingira, hatutasubiri tutasema na hatuko kumfurahisha mtu au kumuonea mtu. Sisi tunataka kuhakikisha tunalinda mazingira,” amesema Mchange.

2 Comments

  • Tuambieni kama kuna sheria. Hamuwezi kutumia matamko ya viongozi kama sheria. Kama zilivyo hadithi, matamko yatapita.
    Sheria hazipitwi na wakati kama ni za vyanzo vya maji na mazingira.
    Mkakampeni kupata sheria!

  • Hivi hizi asasi za kiraia kazi zake ni kujipendekeza kwa wakuu wa serikali au kutetea maslahi ya wanachama wake? Acheni kufanya kazi za PR kwani serikali imeajiri watu kibao kwa kazi hiyo. Nyinyi si wasemaji wala si PR meneja wa Ikulu au TRA au TPA au PMO au Tanesco etc

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!