RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019/2020, imebaini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilishindwa kukusanya ushuru wa forodha Sh. 17.28 bilioni, kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 8 Aprili 2021, jijini Dodoma na CAG, Charles Kichere, wakati akitoa muhtasari wa ripoti hiyo, iliyowasilishwa bungeni.
Akielezea changamoto za TRA, CAG Kichere amesema katika kipindi hicho, TRA ilishindwa kukusanya ushuru wa forodha wa Sh. 5.14 Bilioni wa biadhaa zilizopita kwenda nje ya nchi.

Bidhaa hizo zilipitishwa katika mipaka ya Tunduma, Kasumulu, Rusumo, Kabanga, Mutukula, Namanga, Holili na Kigoma.
“Katika ukaguzi wangu wa bidhaa zinazopita nchini kuelekea nchi jirani, kupitia mipaka ya forodha kwa kuangalia mfumo wa TANCIS na nyaraka za kusafirishia, sikuthibitisha kuwa bidhaa zenye makadirio ya kodi ya forodha Sh. bilioni 5.14 zilitoka nchini,” amesema CAG Kichere.
Mbali na bidhaa hizo kupitishwa nje ya nchi bila kulipiwa ushuru wa forodha, CAG Kichere amesema, TRA ilishindwa kukusanya ushuru wa forodha wa Sh. 12.14 Bilioni wa mafuta yaliyopitiliza muda wake, ambayo yalipaswa kwenda nchi jirani.
Leave a comment