May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CAG agusa nyufa ofisi ya DPP

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Spread the love

 

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20, imebaini kasoro ya kisheria na kikanuni ya matumizi ya fedha zinazotokana na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ripoti hizo 21 za kaguzi mbalimbali, zimewasilishwa leo Alhamisi tarehe 8 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma na CAG, Charles Kichere ambaye baadaye alizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, alipitia uendeshwaji wa akaunti ya fedha zinazotokana na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa serikalini zilizo chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020.

“Nilibaini kuwapo kwa bakaa ya fedha Sh.51 bilioni kutokana na kesi zilizomalizika katika mahakama mbalimbali kwa kipindi cha miaka sita na zaidi,” amesema Kichere.

“Kutotumiwa kwa bakaa ya fedha katika akaunti, kunasababishwa na kutokuwapo kwa sheria na kanuni za kudhibiti matumizi ya fedha itokanayo na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa serikalini,” amesema

CAG Kichere amesema “ni maoni yangu, kuwapo wa fedha zisizotumiwa kwa sababu ya kukosekana kwa muongozo au mfumo wa kisheria kunaweza kusababisha matumizi mabaya ya Fedha za umma na ucheleweshaji wa maendeleo ya umma.”

error: Content is protected !!