Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tani 5,623 za salfa zawasili bandari Mtwara, wakulima wamshukuru Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Tani 5,623 za salfa zawasili bandari Mtwara, wakulima wamshukuru Rais Samia

Spread the love

BANDARI ya Mtwara pamoja na wakulima wa korosho wameendelea kupata neema baada ya tarehe 24 Juni mwaka huu kupokea meli nyingine kubwa iliyobeba viuatilifu aina salfa tani 5,623. Anaripoti Gabriel Mushi, Mtwara … (endelea).

Meli hiyo aina ya ‘boss seven’ iliyopakia mzigo kutoka nchini Uturuki ni neema nyingine kwa bandari ya Mtwara ambayo pia imekuwa ikitumika kusafirisha makaa ya mawe yanayochimbwa kutoka mkoani Ruvuma.

Shehena ya salfa ikishushwa katika meli aina ya Boss 7 iliyotokea nchini Uturuki na kutia nanga katika bandari ya Mtwara Juni 24 mwaka huu. Salfa hiyo tani 5,623 hiyo inatarajiwa kugawiwa bure kwa wakulima wa korosho nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara, Mkuu wa mkoa huo, Meja Jenerali Marco Gaguti amesema viuatilifu hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa korosho na kuinua uchumi kwa wakulima hao.

“Meli hii imefika na viatilifu salama na sasa kilichobaki ni kuanza kusambaza viuatilifu hivi ambavyo tunahakika baada ya siku tatu wakulima wataanza kugawiwa.

“Namhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kwamba pembejeo hizo zimefika mahali pake, wakulima wa zao hili wamefurahi sana kwani wanagawiwa bure,” amesema.

Pia anaagiza watu wote watakao husika katika ugawaji wa pembejeo hizo kuzigawa kwa wakati na bila upendeleo ili kila mkulima afaidike na pembejeo hizo.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Meja Jen. Marco Gaguti akizungumza na waandishi wa habari.

“Rai yangu wito kwa watendaji wa mamlaka za wilaya na hasa kwenye kata ambako kuna zile kamati za pembejo za kata na vijiji, mzigo huu ufike kama ulivyokusudiwa na maelekezo na muongozo nimeshayatoa ili viuatilifu hivi viwafikie wakulima kama ilivyokusudiwa,” amesema.

Aidha, Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Norbert Kalembwe anasema ujio wa meli hizi unawawezesha kuboresha uchumi wa mkulima na bandari kwa ujumla kwani hata maisha ya mtu mmoja mmoja yanaboreshwa.

Amesema mafanikio hayo yanatokana pia na upanuzi wa gati katika bandari hiyo ambao ulikalimika Disemba 2020.

Amesema ujezi huo uliogharimu Sh bilioni 157.8, umewezesha bandari ya Mtwara sasa kuhudumia tani milioni moja kwa mwaka kutoka tani 400,000 za awali.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred amesema mwaka jana walipata ruzuku ya lita milioni 1.4 za dawa za maji pamoja na salfa tani 13,000 ambazo ziliongeza uzalishaji kutoka tani 210,000 mpaka tani 240,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.

Amesema ongezeko hilo limeongeza mapato kwenda kwa wakulima kutoka Sh bilioni 478 hadi 498 mwaka huu.

Amesema kutokana na ruzuku hiyo, lengo la mwaka huu ni kuongeza uzalishaji kutoka tani 240,000 hadi tani 400,000.

Aidha, baadhi ya wakulima nao wameeleza kufaidika na ruzuku hiyo ambayo wanasema imewa-‘boost’ kuendeleza kilimo hicho cha korosho kwa nguvu na ari kubwa.

Mmoja wa wakulima hao mkazi wa mtaa wa Namkundi, kata Magengeni mkoani humo, Saila Abdallah maarufu kama ‘tall’ amesema ruzuku hiyo imempunguzia gharama za kuhudumia shamba lake ambalo lina hekari 27.

“Toka mama (Rais Samia) ameingia madarakani wakulima toka vizuri kwa sababu nimesomesha mtoto wangu wa kwanza amefika hadi chuo kikuu. Amesomea fani ya madini Dodoma,” amesema.

Aidha, amesema licha ya kupata pembejeo bado wanapata shida ya bei za korosho ambayo kwa msimu uliopita wamedai baadhi ya wakulima waliuza korosho kilo moja kw ash 1400 hadi 1800.

“Ninachomuomba atusaidie tupate benki ya wakulima huku kusini, Kwa sababu zilizopo zimeshindwa kuhudumia wakulima.

“Unajua mmea unahitaji kuoga, kupiga mswaki na huduma zote kama binadamu wengine, vivyo hivyo kwa korosho inahitaji kuhudumiwa namna hiyohiyo, kiujumla mambo mengine yote yapo vizuri kwa sababu nimepata dawa na salfa lakini sasa kusafisha gharama za shamba na bei ndio shida.

Mkulima wa korosho katika mtaa wa Namkundi, kata Magengeni mkoani Mtwara, Saila Abdallah maarufu kama ‘Tall’ akizungumzia ruzuku ya pembejeo ilivyomnufaisha.

“Yaani ni sawa na kusema mama ameupiga mwingi lakini kufunga goli bado. Kwa sababu mhudumu wa shamba anahudumia mkorosho kwa sh 300 na mikorosho ipo 1000,” amesema.

Pia amegusia suala la uhaba wa maofisa ugani, ambapo anasema katika kata moja kuwa na ofisa mmoja inamuwia vigumu kuwafikia wakulima wote kwa wakati.

Hoja hizo zinaungwa mkono na mkulima mwingine kutoka Rashid Kamtumba kutoka mtaa wa Pachoto B, Manispaa ya Mtwara mwenye hekari 10.

Amesema angalau bei ya zao hilo kwa kilo moja iongezwe kufikia Sh 3500 hadi 4000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!