Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Ripoti:Viwanda haviweki virutubishi
Tangulizi

Ripoti:Viwanda haviweki virutubishi

Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini, Sarah Gordon akimkabidhi ripoti ya sensa ya viwanda vya kusindika vyakula, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe.
Spread the love

ASILIMIA 90 ya viwanda 33,000 vya kusindika vyakula vilivyofanyiwa sensa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) vimebainika kutoweka virutubishi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamesemwa mwisho mwa wiki jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini, Sarah Gordon wakati akikabidhi ripoti ya sensa ya wamiliki wa viwanda vya kusindika vyakula kwa Naibu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe.

Gordon alisema viwanda vingi vinavyosindika vyakula vina mashine za zamani, hali ambayo inakwamisha kuweka virutubishi muhimu kwenye vyakula vya binadamu.

“WFP tulifanya sense kwenye viwanda 33,000 ambapo zaidi ya asilimia 90 ya viwanda hivyo haviweki virutubishi muhimu, hali ambayo inaondoa msingi mzuri wa kuboresha afya za wananchi hasa watoto,” alisema.

Mwakilishi huyo alisema katika sense hiyo walibaini kuwa viwanda vingi vinamilikiwa na watu wenye miaka kuanzia 36 hadi 55, huku asilimia 7 ya mashine hizo zinamilikiwa na wanawake.

Alisema katika viwanda hivyo vya kusindika vyakula kuna wafanyakazi 1,091 ambapo asilimia 25 ni wanawake na 75 wanaume, huku wamiliki wengi wakiwa ni sekta binafsi.

“Pia sensa hii imebaini katika viwanda hivyo 33,000 asilimia kubwa vinazalisha vyakula vya mahindi, na vinatumia nishati ya umeme kama nyenzo muhimu ya uzalishaji,” alisema.

Mwakilishi huyo alisema WFP Tanzania imefanya sensa ya kina kuhusu viwanda vya ngano na viazi ili kuwa na taarifa sahihi na nafasi ya mazao hayo, yanapopatikana, usambazaji wake, kiasi, virutubishi na uhitaji.

Gordon alisema lengo ni kuhakikisha usalama na lishe inakuwepo kwenye chakula hapa nchini, huku akiweka bayana kuwa WFP Tanzania imefanikisha zoezi hilo kwa taasisi ya OpenMap Development Tanzania (OMDTZ) kwa kusimamiwa na Kitengo cha Lishe na Ubunifu.

“Sensa hii iligawanyika katika sehemu tatu ambapo mosi ilikuwa ni kuzunguka kwenye viwanda, kufanya kazi, na kukusanya taarifa, ambapo zoezi limeenda vizuri hadi leo tunatoa ripoti hii, muhimu kwa afya na maendeleo ya jamii,” alisema.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Naibu Waziri Kigahe alisema imesaidia kutoa takwimu ambazo zitakuwa muongozo kwa Serikali kujua pa kuanzia katika eneo hilo la virutubisho.

Naibu Waziri alisema pia ripoti hiyo inatoa picha sahihi ya idadi ya ajira zilizopo kwenye viwanda hasa vya kusindika vyakula na kwanini haviweki virutubishi.

“WFP wamefanya jambo muhimu sana kwani ni dhahiri kuwa kwa sasa tunamwanga kuhusiana na hali ya uwekeji virutubishi kwenye vyakula, ila pia ajira, teknolojia na mengine ambayo yanahusina na sekta hiyo ya viwanda, alisema.

Alisema Serikali itakuwa inachukua hatua awamu kwa awamu ili kuhakikisha sekta hiyo inafankiwa kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!