Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tanga kujenga Kituo cha Mifupa
Afya

Tanga kujenga Kituo cha Mifupa

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema mkoa wake unakusudia kuanzisha kituo cha Mifupa (Orthopaedic Centre) kwa ajili ya watu wanaopata ajali katika Barabara ya Mkata-Handeni na wakazi wa Tanga kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Malima amesema hayo wilayani Handeni leo tarehe 27 Februari, 2022 alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya hiyo jana.

“Hii ndiyo njia kubwa baada ya hapa watu wanaopata ajali Dar es Salaam kituo cha kwanza labda ukatibiwe Tumbi (Kibaha mkoani Pwani), lakini ukishavuka Chalinze pale hakuna kituo kingine hadi unafika Tanga zaidi ya KCMC.

“Kwa hiyo tunataka hapa katikati tuwe na kituo cha kusaidia wanaopata ajali ambayo ni dharura. Kwa hiyo tumekubaliana, tumejenga hoja Wizara ya Afya imetusikia, Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) imetusikia kwa hiyo tujenge kituo pekee kitakachokuwa baina ya Tumbi na KCMC.

Lakini wakati tunazungumzia kituo hicho hili jengo lilitakiwa liwe limekwisha sasa tutakuwa tunafanya kama ulafi fulani maana unakuwa kama unaomba chakula kingine wakati ulichokuwa nacho hakijaisha huo ni ulafi,” amesema.

Malima amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutaamua hatima ya kituo hicho cha mifupa kwani nia ya kuwa nacho ni kubwa kutokana na umuhimu wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!