October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tambwe Hizza afariki dunia

Richard Tambwe Hizza, enzi wa hai wake akiwa jukwaani katika moja ya kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni

Spread the love

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umepata pigo kutokana na kifo cha mwanasiasa machachari, Richard Tambwe Hizza. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Ukawa ni muunganiko wa vyama vinne, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR Mageuzi pamoja na NLD.

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kifo hicho akisema Hiza amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Mbagala Kuzuiani jijini Dar es Salaam akiwa amelala.

Hiza amefariki kipindi ambacho alikuwa katika timu ya kampeni za kama Mratibu wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge wa Chadema katika Jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na jana jioni alipanda jukwaani.

Kwa upande wake Mwalimu amesema: “Tambwe alikuwa mtu muhimu sana katika timu yangu ya kampeni, kaniacha kipindi muhimu sana.”

Mwalimu amesema kuhusu kuendelea kwa kampeni anasubiri maamuzi ya chama chake lakini yeye binafsi hadhani kama ataweza kuendelea na kampeni kwa kipindi hiki.

Tambwe Hizza, alijiunga na Chadema mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akitokea CCM ambako aliwahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama hicho tawala.

Kabla ya kujiunga na CCM alihama kutoka katika Chama cha Wananchi (CUF) ambako pia alihamia kutoka NCCR-Mageuzi.

MwanaHALISI Online itakuwa karibu

error: Content is protected !!