CHAMA cha Chadema kimehusisha tukio kutekwa kwa mgombea wa udiwani wa kata ya Buhangazi wilayani Muleba Mkoani Kagera, Nelson Makoti kuwa ni njama za kisiasa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji ameeleza kuwa kutekwa kwa diwani huyo ni njama za siasa kutokana na viashiria vya kulazimishwa mgombea huyo kuwa ajiengue kwenye kinyang’anyoro hicho na kwamba atapewa shilingi milioni nane.
Mashinji ameleeza kuwa kiashiria kingine ni kulazimishwa ni kupigiwa simu kwa ndugu zake na mtu aliyetambuliwa kama John Rutenga ambao walishawishi kusihi kutoendelea na uchuguzi huo.
Amesema kuwa mgombe huyo alitekwa alipokuwa akitoka Bukoba Mjini alipokwenda kwa ajili ya kununua vifaa vya kampeni ambapo aliingizwa kwenye gari na kufungwa kitambaa cheusi.
Mashinji ameeleza kwa mujibu wa muhanga wa tukio hilo kuwa aliteswa na kulazimishwa kuacha kugombea nafasi hiyo.
Amesema ndugu na wanachama wa Chadema walikwenda kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Buhangaza ambapo askari wa kituo hicho walisema kuwa tukio hilo ni kubwa hivyo waende kituo cha wilaya ya muleba ambako na huko walinyimwa (RB).
Mashinji ameshangazwa na kitendo cha jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa chama hicho ilhali gari iliyofanya tukio hilo ipo na mmliki wake anajulikana.
Leave a comment