Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtoto yatima abakwa na kukatishwa ndoto zake
Habari Mchanganyiko

Mtoto yatima abakwa na kukatishwa ndoto zake

Spread the love

MMOJA kati ya waathirika wa vitendo vya ubakaji ni motto wa umri wa miaka 13 (jina limehifadhiwa) anayedaiwa kubakwa na kijana anayeitwa Baraka Tendega, wote wakazi wa Mtaa wa Ulonge katika Manispaa ya Iringa. Anaripoti Faki Sosi, Iringa … (endelea).

Kwa mujibu wa Bi. Otevya Mwaluke, shangazi wa mtoto aliyebakwa, kitendo hicho alifanyiwa na kijana anayejulikana mtaani kwao, lakini hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.

Bi Mwaluke amesema kuwa mtoto huyo ambaye ni yatima amepata ujauzito na hivyo kukatiza masomo yake ya elimu ya sekondari baada ya kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka jana na kisha kukutiza masomo yake kutokana na ujauzito.

“Ndoto za mtoto wangu wa pekee niliyeachiwa na kaka yangu amebakwa na kupata ujauzito. Nasikitika amekatiza masomo yake”, amesema Bi. Mwiluke huku machozi yakimlenga.

Amesema kuwa daktari alithibitisha kwamba mtoto huyo amebakwa na hivyo jeshi la Polisi lilichukua hatua ya kumkamata kijana huyo pamoja ambaye yupo nje kwa dhamana.

Bi Mwaluke amesema kuwa yupo tayari endapo sheria itaruhusu kumalizana na kijana huyo asaidiewe ili aweze kumlea mtoto wake.

“Sioni faida ya kufungwa kwa kija a huyo kwa sababu akifungwa mimi nitapata nini huyo mtoto atalelewa na nani,” amesema Bi. Mwiluke, na kuongeza kuwa yupo tayari kukaa meza moja na familia ya huyo kijana kama sheria utaruhusu kwa sababu anaona ndoto za mtoto huyo zimeshakatishwa.

Hata hivyo Bi. Otevya amesema kwa kuwa mtoto huyo anapenda kusoma, ameamua kumpeleka shule inayomilikiwa na Kanisa ili ajifunze masomo ya Kidato cha kwanza pamoja na kumjenga kisaikolojia Bi Otevya anaishi yeye pamoja na mtoto huyo hadi sasa.

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti mkoani Iringa, Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka maafisa wa jeshi hilo kote nchini kupambana vikali na vitendo hivyo vya ubakaji hususani kwa watoto wadogo.

Aidha IGP Sirro amewaonya maafisa wa jeshi la polisi wanaohusika kufuta kesi za ubakaji na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi bila sababu za msingi kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa kanuni na taratibu za jeshi hilo.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Iringa mwishoni mwa mwaka jana ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi zenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona na namna ya kuwasaidia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!