Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Michezo Taifa Stars, Burundi kuchimbika
Michezo

Taifa Stars, Burundi kuchimbika

Spread the love

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Burundi Sadio Berahino amesema wako tayari kuwakabiri timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa siku ya Jumapili 11 Oktoba, 2020 huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa kwenye mchezo waliokutana mara ya mwisho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ambao upo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) utapigwa majira ya saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezaji huyo amezungumza hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kusema kuwa walipokuja hapa mara ya ya mwisho walikuwa na timu nzuri ila walipoteza mchezo kwa njia ya penati.

“Mara ya mwisho tulikuwa hapa na timu iliyokuwa na vijana yenye ubora, tukakosa bahati kwa kupoteza mchezo kwa njia ya penati ila tunaangalia mbele hasa kwenye mchezo wa siku ya Jumapili,” alisema nahodha huyo. 

Mchezaji huyo ambaye ni tishio kwenye kikosi cha Burundi kwa sasa anacheza klabu ya Zulte Waregem inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, pia aliwahi kupitia kwenye klabu za Stock City na West Bromwich Albion inayoshiriki Ligi kuu nchini England.

Kwa upande wa Nahodha msaidizi wa kikosi cha Taifa Stars, Aishi Manura amesema kuwa wamejipanga vizuri kwenye mchezo huo wa siku ya Jumapili na kuwataka watanzania kuja kuishangilia na kuisapoti timu yao katika mchezo huo.

“Kwa niaba ya wachezaji kiujumla tuko vizuri na tumejiandaa na pambano dhidi ya majirani zetu Burundi, itakuwa mechi ngumu na ushindani kwani mar azote tukicheza nao zinakuwa mechi ngumu,” alisema Manula

Aidha Manula amesema kuwa mchezo huo kumpa heshima Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Hayati Benjamini Willium Mkapa kwa kuwa timu hiyo itakuwa inacheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja huo toka ulivyobadilishwa jina.

Mchezo huo utakuwa kipimo kwa kocha wa kikosi cha Taifa Stars Etiene Ndayiragije kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia unaotarajiwa kuchezwa 13 Novemba, 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

error: Content is protected !!