Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea ubunge Ubungo abadili mbinu za kampeni
Habari za Siasa

Mgombea ubunge Ubungo abadili mbinu za kampeni

Eugine Kabendera, Katibu Mkuu wa Chaumma Bara
Spread the love

KABENDERA Eugene, Mgombea wa Ubunge wa Ubungo kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), amefanya kampeni ya aina yake kupitia mkutano na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kabendera amefanya kampeni hiyo leo Ijumaa tarehe 9 Oktoba 2020 akisema, ameamua kutumia njia hiyo ya kipekee kwasababu hakuna muongozo wa kuomba kura kwa wananchi licha ya kuwa na neno moja tu la kampeni.

“Natumia haki yangu ya msingi kama mgombea, naongea na waandishi wa habari kwa maana naamini mnafika kwa watu wengi zaidi, kampeni nafanya na kama mtu anaona akifunga jukwaa katika eneo fulani ndo amefanya kampeni sijui! na kama amefanya tathmini kafikia watu wangapi nani anajua?” amesema.

Amesema, amefanya kampeni za nyumba kwa nyumba mara kadhaa na mabango amebandika lakini kwa njia hiyo, anaamini anafikia watu wengi wa kutosha.

Katika kampeni hiyo, Kabendera ameendelea kusisitiza, suala la ubwabwa mashuleni na mahospitali bado lipo palepale kama sera kuu ya chama hicho.

Amesema, endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anasimamia suala la upatikanaji wa chakula mashuleni na hospitali, mikopo kwa wanafunzi isiyokuwa na riba pamoja na kutetea mabadiliko ya sheria zinazosimamia mitandao ya simu.

Kabendera ambaye pia amewahi kuwa Katibu Mwenezi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, suala hilo ni la msingi hivyo halina mjadala na hata kama serikali inayokuja itakuwa ngumu kukubalina nalo atahakikisha halmashauri ya Ubungo inasimamia kutenga bajeti katika shule za serikali za ubungo watoto wapate chakula asubuhi na mchana ili kukamilisha dhana ya elimu bure.

“Mtoto akiwa na njaa hafundishiki, nichagueni twende pamoja ili vita yangu ya kwanza nikapiganie na inawezekana ndani ya miaka mitano kabisa” amesema.

Aidha, amesema ajenda yake nyingine ni kutatua changamoto ya ajira katika jimbo hilo kwa akina mama na vijana.

“Jimbo la ubungo lilikuwa na viwanda kuna urafiki na viwanda kadhaa lakini vimedorora ama kufungwa, tunahitaji mtu atakayepiga kelele za kutosha na kuleta wawekezaji wakavifufua”

Amesema, katika suala la ajira vijana wengi hawajapata mikopo ya halmashauri ambayo lengo lake ni kuinua hali ya vijana kujiajiri na kuhakikisha inabaki kuwa na sifa ya halmashauri bila kuwa na dhama kama mikopo ya benki.

“Ukinunua umeme wa Sh.1,000 kama haujawasha taa ukisafiri hata mwaka utaukuta lakini hawa wenzetu wa mitandao ya simu ukiweka Sh.1,000 ukajiunga kifurushi cha siku na unaotaka hawapatikani ikipinduka siku ya piki hela itaondoka bila kuitumia, haya hayawezi kubadilika bila kuwa na wasemaji” amesema Kabendera.

Amesema serikali lazima ifikilie kupunguza kodi za mawasiliano kuanzia gharama za intaneti hadi za kupiga simu kwakuwa huduma hiyo kwa sasa ina uhitaji mkubwa kama ilivyo kwenye maji na umeme.

Sera nyingine za Kabendera ni pamoja na kutengeneza mfumo rasmi makazi ya wanafunzi wa vyuo vilivyopo ndani ya Ubungo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!