Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa IGP Sirro atoa onyo Z’bar ‘tusikubali kutumiwa’
Habari za Siasa

IGP Sirro atoa onyo Z’bar ‘tusikubali kutumiwa’

IGP Simon Sirro
Spread the love

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro, amewataka Wazanzibar kufuata taratibu za upigaji kura zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ili kuepusha kuingia matatani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

ZEC imeweka utaratibu wa upigaji kura wa uchaguzi mkuu visiwani humo kufanyika kwa siku mbili tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Leo Ijumaa, tarehe 9 Oktoba 2020, IGP Sirro amezungumzia uchaguzi huo akisema, kuna watu wako ndani wanasota kwa makosa ambayo “mimi naamini wametumwa na viongozi wa siasa baadhi ambao wao wanaendelea kula kuku tu mitaani wewe unapata shida gerezani.”

“Hili la tarehe 27 Oktoba ambapo Zanzibar kwa mujibu wa kanuni zilizopo wafanyakazi wa serikali wataanza kupiga kura na tarehe 28 Oktoba ni kura za watu wote.”

Dk. Hussein Mwinyi, Mgomnbea Urais Zanzibar (CCM)

“Nimesikia kuna kuhamasisha tarehe 27 Oktoba wote wakapige kura, niwaombe ndugu zangu wa Zanzibar sheria, kanuni na taratibu zote, tuzifuete kama zilivyowekwa na ZEC,” amesema IGP Sirro

Katika kusisitiza, IGP Sirro amesems “tusikubali kutumiwa na kikundi cha watu kwa ajili ya kuvunja sheria, atakayepata shida ni wewe utakayekwenda tarehe 27 Oktoba badala ya 28 Oktoba na najua kuna vikundi vimeandaliwa kwa ajili ya kuleta hilo tatizo lakini niwahakikishie uwezo huo hawana.”

Amesema, “imani yangu tutapiga kura kwa amani na utulivu na mwisho tutapata viongozi wanaowataka.”

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Hili si onyo la kwanza kwa IGP Sirro kulitoa visiwani humo, kwani amewahi kuwaonya wale wote watakaojaribu kuvuruga uchaguzi huo, watachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema, ili kuhakikisha hali hiyo inadumishwa, ataweka kambi siku ya upiga kura ili kujionea hali itakavyokuwa.

2 Comments

  • Huyu siro anawatisha Wazanzibari tu arnde akapambane na LISSU huko kwao bara. Saa ya UKOMBOZI inakuja uhuru kamili kupatikana 28/10

  • SIASA SIOCHUKI, SIO UADUI,NAWALA SIASA SIOUBABE, TUKUMBUKE KWAMBA, KUNAMAISHABAADA YAUCHAGUZI, KWAPAMOJA, TUTAIJENGA TZ.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!