Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu TADB yawashika mkono wahitimu waliofanya vizuri SUA
ElimuHabari Mchanganyiko

TADB yawashika mkono wahitimu waliofanya vizuri SUA

Spread the love

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewapongeza wahitimu bora wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) cha Morogoro kwa kuwapatia zawadi ya fedha taslimu Sh milioni tano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Motisha hiyo ya fedha, imetolewa na TADB kama sehemu ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kupitia mpango mkakati wake mpya uliozinduliwa mwaka huu.

Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Jacqueline Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro Prof Raphael Chibunda muda mfupi baada ya kumtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya namna taasisi hizo mbili zinaweza kuendelea kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri na wafanyakazi katika eneo la utafiti, Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa TADB, Jacqueline Minja alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Benki yetu inatambua uwepo wa mikakati mbalimbali ya serikali kama vile sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambayo imetilia mkazo umuhimu wa kuweka mazingiza wezeshi kwa vijana kujihusisha na shughuli za kiuchumi, ikiwemo kilimo cha kisasa na kibiashara. Kwa kutambua hili, kwa kuanza, TADB imefika hapa na kutoa tuzo kwa wanafunzi bora mwaka huu.”

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kampasi kuu Morogoro, Prof Raphael Chibunda (katikati) akizungumza na Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Jacqueline Minja (kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa TADB na SUA ofisini kwake.

Afisa rasilimali huyo alieleza kuwa, katika awamu nyingine, benki itaandaa programu maalumu ya kuatamia vijana bora kutoka chuo kikuu cha SUA ilikutoa fursa ya kujifunza kazini.

“Programu hiyo itakayokuwa ya miezi 24, italenga kutoa nafasi kwa wahitimu bora kuweza kupata nafasi ya kujifunza kazi kwa vitendo katika benki yetu,” alieleza Minja.

Wafanyakazi wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu bora wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 5 kwa wanafunzi hao kuwapongeza kwa juhudi walizoonesha katika masomo yao.

Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkuu wa Chuo Prof Raphael Chibunda aliishukuru TADB kwa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pamoja na mpango wake wa kuandaa programu maalum ya kuwaatamia wahitimu wa fani ya kilimo.

TADB itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) katika juhudi za kutengeneza vijana wabobezi katika sekta ya kilimo ili kuwezesha vijana kuchangia kufikia malengo ya serikali ya ‘Agenda 10/30’.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!