November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba wapewa Wazambia kombe la Shirikisho

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imepangiwa kumenyana na kikosi cha Red Arrows ya kutoka nchini Zambia, kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Simba imeangukia kwenye michuano hiyo, mara baada ya kutupwa nje na Jwaneng Galaxy, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa faida ya bao la ugenini mara baada ya kwenda sare ya mabao 3-3, kwenye michezo yote miwili.

Kwenye michuano hiyo ya kombe la Shirikisho, ambapo Droo yake imechezeshwa hii leo mchana tarehe 26 Oktoba, jijini Cairo nchini Misri.

Mchezo wa kwanza Simba itaanzia nyumbani tarehe 28 Novemba, 2021, na kisha Desemba 5, 2021 utachezwa mchezo wa marudiano nchini Zambia.

Red Arrows wamefika hatua hiyo mara baada ya kupata ushindi kwenye michezo yao yote miwili kwenye hatua za awali.

Kwenye mchezo wa kwanza Red Arrows walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Young Buffoloes kwenye michezo yote miwili, na kisha kwenda kumenyana na De Agosto ya Angola.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Zambia, Red Arrows wanashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo mara baada ya kucheza michezo mitano na kuambulia alama 4.

error: Content is protected !!