December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amtembelea Lowassa

Spread the love

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemtembelea nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais Samia amemtembelea Lowassa aliyekuwa waziri mkuu katika utawala wa awamu ya kwanza wa Rais Jakaya Kikwete, leo Jumanne tarehe 26 Oktoba 2021.

Katika ukurasa wa Twitter wa Ikulu ya Tanzania, imeweka picha za Rais Samia, Lowassa na Regina, Mke wa Lowassa wakiwa na nyuso za tabasamu.

Picha hizo zimekwenda na maneno “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa wakati alipo mtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Oktoba 2021. Kushoto Mke wa Mhe. Lowassa Mama Regina Lowassa.”

error: Content is protected !!