November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Shule iliyoshika mkia Sengerema, yazinduka

Spread the love

 

SHULE ya Sekondari ya Kome, iliyopo Buchosa, Wilaya ya Sengerema, Mkoani Mwanza, iliyokuwa ikishika nafasi ya mwisho kwa matokeo mabovu ya katika wilaya hiyo, imezinduka. Anaripoti Mwandish Wetu, Mwanza … (endelea).

Kome iliyokuwa na matokeo mabovu ya Kidato cha Pili na Nne katika mitihani ya kitaifa kwa miaka mitatu fululizo (2017, 2018 na 2019), sasa imefaulisha kwa asilimia 88 Kidato cha Nne na asilimia 97 Kidato cha Pili mwaka 2020.

Imeelezwa, shule hiyo ni miongoni mwa shule 20 za sekondari ziliko katika Halmashauri ya Buchosa, zilizokuwa na matokeo mabaya kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na usimamizi mbovu.

Bruno Sangwa, Ofisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Buchosa, alifanya mabadiliko ya uongozi wa shule hiyo kwa kumuhamisha aliyekuwa mkuu wa shule hiyo, Lukas Lupimo na kuikabidhi kwa mkuu mpya, Dunua Luhula.

Mwaka 2020, shule hiyo Kidato cha Nne imeshika nafasi ya 14 Kati ya shule 20, amba kimkoa ikishika nafasi 195 ya Kati ya shule 241. Katika matokeo ya Kidato cha Pili, imeshika nafasi ya tisa kati ya shule 20.

Shule hiyo ina wanafunzi 1026, walimu 15, vyumba vya madarasa 11 ambapo mahitaji ni vyumba 23 pungufu ikiwa vyumba 12.

Luhula ambaye ndio mkuu wa shule hiyo kwa sasa, aliyehamishiwa hapo tarehe 11 Februari 2020 amesema, tatizo lilikuwa kutowajibika kwa walimu.

“Kuanzia mwaka 2021, mipango yetu ni kuhakisha shule hiyo inashika nafasi za juu kiwilaya na kimkoa, na kuhakikisha tunatokomeza ziro, ” amesema Luhula.

error: Content is protected !!