April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkakati kukabili chanjo bandia wasukwa

Spread the love

 

MKAKATI wa kukabiliana na chanjo bandia ya virusi vya corona (COVID-19), umewekwa na wakurugenzi wa upelelezi wa nchi wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wakuu hao wamekutana kujadili changamoto za mataifa yao, ikiwemo mlipuko wa COVID-19 unaotesa dunia kwa sasa.

Taarifa hiyo imetolewa na IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini baada ya kuufungua mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, tarehe 11 Machi 2021.

Sirro ambaye ni mwenyekiti wa EAPCCO, amesema wakuu hao watajadili namna ya kudhibiti uingizwaji wa chanjo bandia za corona katika nchi hizo.

“Changamoto ya ugonjwa w a corona hiyo bado haijapata utatuzi, kikubwa utakuta changamoto hizi ni barakoa, kutokana na ugonjwa huu wanauza barakoa feki, lakini pia inaonekana kuna baadhi ya chanjo zinazokuja zinakuwa bandia, tuna kazi kubwa sana kukabiliana na hilo,” amesema IGP Sirro.

Sambamba na changamoto za corona, IGP Sirro amesema wajumbe wa mkutano hao wamejadiliana kuhusu masuala ya ugaidi, ukatili wa kijinsia na haki za binadamu.

Amesema baada ya majadiliano hayo, mapendekezo yake yatawasilishwa kwa wakuu wa polisi wa nchi wanachama kwa ajili ya utekelezaji.

“Ajenda kubwa tunaona kuhusu mambo ya ugaidi, kijinsia na haki za binadamu, kuna mambo mengi yatazungumzwa na mwisho wa siku watakuja na maamizimio halafu utekelezaji utaanza lengo ni kuhakikisha nchi zetu 14 zote kuna kuwa salama,” amesema IGP Sirro.

“Watakayo kubaliana kwa ajili ya utekelezaji yataletwa kwetu ambao wakuu wa polisi katika nchi zote 14, lengo kuhakikisha mtu anayefanya kosa katika nchi 14 tunamshughulikia kama mhalifu kwa nchi alizofanya, ukifanya uhalifu Kenya sisi tunakukamata.”

error: Content is protected !!