Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheikh Dodoma ahimiza sensa ya watu na makazi
Habari Mchanganyiko

Sheikh Dodoma ahimiza sensa ya watu na makazi

Spread the love

SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Shaban Rajabu amewahimiza waumini wa dini ya Kiislam kuhakikisha wanashiriki katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agost mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea)

Alhaji Rajabu ametoa wito huo leo tarehe 10 Julai mwaka huu wakati wa ibada maalumu  ya sikuuu ya Eid Al-Adha  pamoja na kuliombea Taifa, Rais wa Nchi, viongozi wa ngazi zote iliyofanyika katika msikiti wa Gadafi jijini hapa.

Amesema suala la kushiriki katika sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa watanzania wote ili kuwasaidia viongozi na serikali jinsi ya kuwasaidia watu wake.

“Suala la kuhesabiwa ni muhimu maana linafanya wepesi kwa viongozi kujua wanaweza kutoa huduma kwa watu wanagapi na uwiano gani ikiwa ni pamoja na kutambua mahitaji ya makundi maalum.

“Watu wote wanatakiwa kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu wa aina yoyote kwani itasaidia viongozi kutambua jamii ya watu hao inahitaji mahitaji yao kwa kiwango gani” amesema Alhaji Sheikh Rajabu.

Katika hatua nyingine Alhaji Sheikh Rajabu amewataka wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao kwa lengo la kuwajengea misingi mizuri ya kimalezi badala ya kuwaacha na kuzagaa mitaani jambo ambalo linasababisha makundi ya uhalifu maarufu kwa jina la ‘panya road’.

Ametoa wasaa huo kwa walezi na wazazi wa watoto wakati akizungumzia na umoja wa wajane wa Dini ya kiislamu ambao wamefika msikitiki hapo kwa ajili ya kupokea sadaka ya kitoweo.

Alhaji Sheikh Rajabu amesema msikiti wa Gadaf umeazisha mfuko wa kuwawezesha wajane na yatima ili kuweza kujikwamua kimaisha.

“Tunatarajia hivi karibuni kuzindua mfuko kwa ajili ya wajane na yatima na tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kutuwezesha Sh. milioni 10 kuanzisha mfuko huo ambao utawawezesha wajane kujishughulisha na masuala ya ujasiriamali” amesema.

Naye Mwenyekiti wa wajane, Rahma Mohammed amesema wajane kama watashikamana na kutumia fursa wanazopata kupitia uongozi wa msikiti wa Gadaf wataweza kujikwamua kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!