MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Kanda ya Ziwa Magharibi imekamata shehena ya sigara bandia zenye thamani ya Sh 1.8 Bilioni katika mkoa wa Shinyanga zikitokea nchini Congo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea)
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TMDA, ofisi ya Kanda ya ZiwaMagharibi ilipokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku lililozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga na baada ya kwenda kuzikagua ikabainika kuwa sigara hizo ni bandia.
Taarifa hiyo iliyotolea leo Jumatano tarehe 28 Septemba, 2022 imeeleza kuwa shehena hiyo ilikuwa na jumla ya makasha 2200 yenye uzito tani 13.2.
“Makasha hayo yana uzito wa tani 13.2 kazi hii tulishirikiana kwa karibu sana na MCIE, lakini cha kujiuliza zimepitaje mipakani na tunao wakaguzi huko? Hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na mzigo huu umezuiliwa,” amesema Gaudensia Simwanza Meneja wa Kitengo cha Uhusiano TMDA.
Leave a comment