Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tume ya madini yawanoa wachimbaji wa madini kwenye maonesho ya madini Geita
Habari Mchanganyiko

Tume ya madini yawanoa wachimbaji wa madini kwenye maonesho ya madini Geita

Spread the love

WATAALAM kutoka Tume ya Madini wameendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini kutoka katika mkoa wa Geita na mikoa ya jirani katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Elimu imetolewa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.

Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi waliotembelea banda la Tume ya Madini wamepongeza  weledi wa wataalam wa Tume ya Madini kwenye utoaji wa elimu na kuwaomba kuendelea na zoezi hilo katika mikoa mingine yenye shughuli za uchimbaji wa madini.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Tume ya Madini, Greyson Mwase amesema kuwa wamejipanga kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote wanaotembelea maonesho hayo pamoja na huduma kama vile upimaji wa madini na kuwaelekeza namna ya kujisajili katika mtandao wa leseni za madini.

“Tumejikita pia kutoa elimu katika eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini (local content) ili wananchi wengi waweze kufahamu fursa zilizopo kwenye migodi ya madini na kuchangamkia kama vile utoaji wa huduma za vyakula, vifaa vya usalama migodini, ulinzi ili nao waweze kunufaika,” amesema Mwase.

Amesema tume imeendelea kuweka mikakati mingine ya kuelimisha umma ikiwa ni pamoja na uandaaji na urushaji wa vipindi vya redio na televisheni, tovuti na mitandao ya kijamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

error: Content is protected !!