Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Serikali yavutiwa na mpango wa Vodacom wa ‘Code like a Girl’
BiasharaHabari za Siasa

Serikali yavutiwa na mpango wa Vodacom wa ‘Code like a Girl’

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

SERIKALI imevutiwa na mpango wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wa ‘Code like a Girl’ na kuahidi kujenga chuo maalum kitachofundisha vijana wa kitanzania masuala ya Teknolojia na Digitali ili kuwaanda na kuyakabili mabadiliko ya teknolojia yanayokuwa kwa kasi nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 15 Februari 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa mkutano wa kujadili mabadiliko ya Teknolojia ulioandaliwa na Kampuni ya Simu ya Vodacom ulioitwa ‘Future Ready Summit’

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameyapokea matamanio ya Vodacom ya kutaka wasichana kupata ujuzi wa teknolojia kwa kujenga chuo cha Tehema.

“Rais Samia Suluhu Hassan amepokea matamanio yenu kwa kushirikiana na mataifa mengine ametenga pesa za kutosha kwa kuanzisha chuo maalum na kulijenga jengo maalum litakalowajumuisha vijana wa kitanzania wanaotamani kujifunza masuala ya kidigitali ili wapate ujuzi na watengeneze fursa mbalimbali kupitia jengo hilo litakaoanza ujenzi muda mfupi katika miaka hii ya bajeti,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza Vodacoma kwa kuwadhamini wasichana 70 kupitia mafunzo ya kidogitali yaitwayo ‘Code like a Girl’ yanayolenga kuwaimarisha kwenye tehema.

“Nimekutana na wasichana wote wanaoendelea na mafunzo wana umri wa kawaida na sio tu hiyo ya Code like a Girl nimekutana na vijana wengine wenyekijifunza masuala ya kiditali.

“Tumesikia kuwa mafunzo hayo yatawafunza wasichana kuanzia umri wa miaka 14 mpaka 19 kwa kufuzu mafunzo haya mnaweza kujiajiri kwa kuanzisha kampuni zenu nanyi mkaajili watu, hii ndio njia tunayoiona namna Vodacom inaweza kuiunga mkono Serikali,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amewatoa hofu wananchi juu ya kupoteza ajira kutokana na ujio wa teknorojia na badala yake amewataka kujipanga kuitumia teknolojia kutengeneza fursa zaidi.

Nape amesema historia ilianza na mapinduzi ya viwanda ambapo pia watu walipoteza ajira lakini walikubaliana na mazingira hayo, hivyo ujio wa teknorojia hayakwepeki muhimu ni kujiandaa na mazingira hayo kwa lengo la kwenda nayo sambamba.

“Nataka kuwatoa hofu watanzania mapinduzi haya hayakwepeki lazima tutakwenda kazi yetu kujipanga namna mzuri ya kujipanga ni pamoja na hii kujadiliana, kuwekeza kwenye ujuzi na kusonga mbele kwa sababu dunia inakwenda huko na sisi hatuwezi kubaki kuwa kisiwa,” amesema Waziri Nape na kuongeza.

“Juzi pale bungeni kulikuwa na mjadala namna akili bandia itakavyokwenda kuathiri uchaguzi na wanasiasa wanafikiri uchaguzi sasa hiyo ilikuwa upande wanasiasa lakini na hakika hata watu wa kawaida wanazungumzia hayo lakini katika kila mapinduzi kuna faida na sisi kama Watanzania tuyabebe.”

Amesema kazi yetu ya kwanza kutengeneza mifumo ya kisheria, ziwezeshe ukuaji na mabadiliko haya ya teknolojia na kazi ya pili ni kuhakikisha uwekezaji kwenye miundombinu ndio maana kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na makampuni ya simu na mfuko wa mawasiliano kunatandaza na kuipandisha hadhi minara huko mikoani pamoja na ujenzi wa mikongo.

Amesema kuwa matokeo ya maendele9 ya Teknolojia yanachagizwa na sera nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan yaliyowavutia wawekezaji nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!